Home Michezo ERIC BAILLY NJE HADI JANUARY MWAKANI

ERIC BAILLY NJE HADI JANUARY MWAKANI

0

************

NA EMMANUEL MBATILO

Beki kisiki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ivory Coast, Eric Bailly atakuwa nje ya uwanja takribani miezi minne mpaka mitano kutokana na majeruhi aliyoyapata hivi karibuni.

Meneja wa klabu hiyo, Ole Gunner Solskjaer amethibitisha mlinzi huyo atakosa mechi karibia nusu msimu hivyo anategemewa kurudi dimbani mwezi January mwakani.

Bailly aliiumia katika mchezo wa kirafiki kwenye michuano ya ICC dhidi ya Tottenham wiki iliyopita.