Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.
Faraji Mnyepe akifafanua jambo kwa wasanii wa sanaa mbalimbali nchini kuhusu fursa za mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wanachama wa SADC, katika kikao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Julai 30, 2019.
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan
Mlawi akifafanua jambo kwa wasanii wa sanaa mbalimbali nchini kuhusu fursa za
mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wanachama wa SADC, katika kikao
kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Julai 30, 2019.
Baadhi ya Wasanii wakifuatilia kikao cha Makatibu Wakuu kutoka Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu Mkutano wa SADC, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Julai 30, 2019.
Rais wa Shirikisho la sanaa za maonesho Tanzania, William Frank Chitanda
akifuatilia kikao cha Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wasanii kuhusu mkutano wa SADC, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Julai 30, 2019.
Msanii wa mziki wa kizazi kipya, Peter Msechu, akizungumza katika kikao cha
Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wasanii kuhusu Mkutano Mkuu wa SADC, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Julai 30, 2019.
Msanii wa Sanaa ya uchoraji, Mosses Luhanga, akizungumza katika kikao cha
Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wasanii kuhusu Mkutano wa SADC, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)