Home Michezo ARSENAL KUVUNJA KIBUBU KUMSAINISHA PEPE

ARSENAL KUVUNJA KIBUBU KUMSAINISHA PEPE

0

***********

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza ipo mbioni kukamilisha dili la kumsajili Mshambuliaji wa klabu ya Lille ya nchini Ufaransa,Nicolas Pepe.

Klabu zote mbili zimefikia makubaliano kwa ajili ya kumsajili winga huyo raia wa Ivory Cost kwa ada ya £72M.

Sasa mazungumzo kati ya Arsenal na wawakilishi wa Pepe yanaendelea na Arsenal wana uhakika wa kukamilisha dili hilo masaa machache baadae.

Inasemekana Arsenal watalipa pesa hizo kwa awamu katika mkataba wa miaka mitano yote.

Klabu kadhaa zimekuwa zikimfukuzia winga huyo zikiwemo klabu ya Napoli,Liverpool na Manchester United lakini klabu ya Arsenal ndio imekuwa na uhakika wa kuinasa saini ya mchezaji huyo.