Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameagiza Mwongozo wa Kutambua na Kuendeleza Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa Asilia uhuishwe ili kuwa na wigo mpana wa kutambua wabunifu kuwezesha na kuwaendeleza.Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Ubunifu cha kampuni ya Jematech ambapo amesema miongozo iliyopo na inayoandaliwa iwe ya rahisi na shirikishi.Aidha amesema muongozo uliopo wa kutambua wabunifu uhuishwe ili kutoa nafasi pana zaidi kwa bunifu mbalimbali kutambulika kwa taratibu rahisi na rafiki kwa wadau badala ya kuwa na taratibu ngumu za kuwakatisha tamaa na kushindwa kuendelea na bunifu zao.“Tumepewa dhamana ya kusimamia masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu sisi tusiwe kikwazo kwa watu ambao wanamawazo mazuri bali tuwe wawezeshaji ili tuwawezeshe ndoto na bunifu zao kunufaisha watanzania” amesema Ndalichako.Akizungumzia kituo hicho Prof. Ndalichako amesema amefarijika kuona kampuni ya Jematech imeamua kuwekeza na kuendeleza ubunifu nchini kwa kuanzisha kituo cha teknolojia jijini Mwanza, kwani ni cha kisasa kizuri chenye miundombinu na vifaa vya kisasa vya kiteknolojia.Amesema amefarijika kuona kituo cha Jema kinatoa fursa kwa vijana wa kitanzania wenye ubunifu kutumia miundo mbinu ya kituo hicho na pia kupata nafasi ya kujifunza na kuendeleza mbunifu zao huku haki miliki ya bunifu kubaki kwa vijana hao.“Kwa hiyo watatoa fursa kwa vijana wanaojihusisha na ubunifu wa kijiditali kuweza kujiendeleza na kutatua changamoto mbalimbali katika jamii yetu na nimefarijika sana kuona tayari wanatoa fursa kwa wanafunzi waliopo vyuo vikuu vyetu kutumia kituo chao bure na kuwa watatoa ushauri na kuwasaidia kiendeleza bunifu zao, huu ndio utekelezaji wa dhani shirikishi na srkta binafsi amesema Waziri Ndalichako”Aidha, Profesa Ndalichako ameitaka Tume ya Sayansi na Teknolojia kubadilika kwa kutambua kuwa ubunifu ni mtu kufanya kitu ambacho ni zaidi ya kile unachofanya ama kukijua na kutambua kuwa sekta binafsi ina mchango katika kuendeleza teknolojia na ubunifu hivyo washirikiane nao kwa karibu.Ndalichako amepongeza Vijana waanzilishi wa Kampuni hiyo hapa nchini akiwemo Mkurugenzi Mtendaji na Injinia Mkuu ambao ni zao la shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma walipata nafasi ya kwenda kusoma na kuishi nje ya nchi lakini wameamua kurudi na kutumia ujuzi walioupata kuendeleza nchi yao.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema ajira kubwa sasa iko katika eneo la teknolojia kwenye TEHAMA ambapo amesisitiza ndiko duniani inakokwenda.Mongella amesema kama Taifa kuna kazi kubwa ya kujenga vituo vya ubunifu kwani mpaka sasa haijawekezwa vya kutosha. Amemuomba Waziri Ndalichako kusimamia hilo ili kutoa fursa kwa vijana wengi kote nchini wenye ubunifu mkubwa ila hawajapata fursa ya kuziendeleza.Awali Mkurugenzzi Mkuu wa Jematech Jumanne Mokili alimweleza Waziri kuwa Kituo hicho kinalenga kutumia mawazo ya pekee, fursa raslimaliwatu na vitu vinavyopatikana nchini kutatua changamoto katika jamii na kwa kutumia teknolojia na ubunifu.Amesema lengo la Jema ni kuiona Tanzania kuwa kampuni kubwa yenye kuleta ushindani katika makampuni makubwa Duniani ya teknolojia na ili kutimiza hilo unahitajika uwekezaji madhubuti na dhati wa rasilimaliwatu, hivyo imewaleta pamoja wahandisi wake waliopo Tanzania, Japan na Marekani ili kubadilishana ujuzi na kubuni mifumo itakayotatua changamoto za kimfu
mo katika maeneo ya kilimo, afya ,elimu na biashara chini .
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameagiza Mwongozo wa Kutambua na Kuendeleza Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa Asilia uhuishwe ili kuwa na wigo mpana wa kutambua wabunifu kuwezesha na kuwaendeleza.
Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Ubunifu cha kampuni ya Jematech ambapo amesema miongozo iliyopo na inayoandaliwa iwe ya rahisi na shirikishi.
Aidha amesema muongozo uliopo wa kutambua wabunifu uhuishwe ili kutoa nafasi pana zaidi kwa bunifu mbalimbali kutambulika kwa taratibu rahisi na rafiki kwa wadau badala ya kuwa na taratibu ngumu za kuwakatisha tamaa na kushindwa kuendelea na bunifu zao.
“Tumepewa dhamana ya kusimamia masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu sisi tusiwe kikwazo kwa watu ambao wanamawazo mazuri bali tuwe wawezeshaji ili tuwawezeshe ndoto na bunifu zao kunufaisha watanzania” amesema Ndalichako.
Akizungumzia kituo hicho Prof. Ndalichako amesema amefarijika kuona kampuni ya Jematech imeamua kuwekeza na kuendeleza ubunifu nchini kwa kuanzisha kituo cha teknolojia jijini Mwanza, kwani ni cha kisasa kizuri chenye miundombinu na vifaa vya kisasa vya kiteknolojia.
Amesema amefarijika kuona kituo cha Jema kinatoa fursa kwa vijana wa kitanzania wenye ubunifu kutumia miundo mbinu ya kituo hicho na pia kupata nafasi ya kujifunza na kuendeleza mbunifu zao huku haki miliki ya bunifu kubaki kwa vijana hao.
“Kwa hiyo watatoa fursa kwa vijana wanaojihusisha na ubunifu wa kijiditali kuweza kujiendeleza na kutatua changamoto mbalimbali katika jamii yetu na nimefarijika sana kuona tayari wanatoa fursa kwa wanafunzi waliopo vyuo vikuu vyetu kutumia kituo chao bure na kuwa watatoa ushauri na kuwasaidia kiendeleza bunifu zao, huu ndio utekelezaji wa dhani shirikishi na srkta binafsi amesema Waziri Ndalichako”
Aidha, Profesa Ndalichako ameitaka Tume ya Sayansi na Teknolojia kubadilika kwa kutambua kuwa ubunifu ni mtu kufanya kitu ambacho ni zaidi ya kile unachofanya ama kukijua na kutambua kuwa sekta binafsi ina mchango katika kuendeleza teknolojia na ubunifu hivyo washirikiane nao kwa karibu.
Ndalichako amepongeza Vijana waanzilishi wa Kampuni hiyo hapa nchini akiwemo Mkurugenzi Mtendaji na Injinia Mkuu ambao ni zao la shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma walipata nafasi ya kwenda kusoma na kuishi nje ya nchi lakini wameamua kurudi na kutumia ujuzi walioupata kuendeleza nchi yao.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema ajira kubwa sasa iko katika eneo la teknolojia kwenye TEHAMA ambapo amesisitiza ndiko duniani inakokwenda.
Mongella amesema kama Taifa kuna kazi kubwa ya kujenga vituo vya ubunifu kwani mpaka sasa haijawekezwa vya kutosha. Amemuomba Waziri Ndalichako kusimamia hilo ili kutoa fursa kwa vijana wengi kote nchini wenye ubunifu mkubwa ila hawajapata fursa ya kuziendeleza.
Awali Mkurugenzzi Mkuu wa Jematech Jumanne Mokili alimweleza Waziri kuwa Kituo hicho kinalenga kutumia mawazo ya pekee, fursa raslimaliwatu na vitu vinavyopatikana nchini kutatua changamoto katika jamii na kwa kutumia teknolojia na ubunifu.
Amesema lengo la Jema ni kuiona Tanzania kuwa kampuni kubwa yenye kuleta ushindani katika makampuni makubwa Duniani ya teknolojia na ili kutimiza hilo unahitajika uwekezaji madhubuti na dhati wa rasilimaliwatu, hivyo imewaleta pamoja wahandisi wake waliopo Tanzania, Japan na Marekani ili kubadilishana ujuzi na kubuni mifumo itakayotatua changamoto za kimfu
mo katika maeneo ya kilimo, afya ,elimu na biashara chini .
mo katika maeneo ya kilimo, afya ,elimu na biashara chini .