Home Mchanganyiko Maafisa Michezo Nchini Watakiwa Kusimamia Michezo na Sio Kukaa Ofisini

Maafisa Michezo Nchini Watakiwa Kusimamia Michezo na Sio Kukaa Ofisini

0

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA), Edward Kapopo akisisitiza jambo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akifungua kongamano la wadau wa michezo mapema hii leo Julai 26,2019 Mjini Mtwara.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA), Edward Kapopo (kulia) akimkabidhi mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza risala ya chama hicho wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akifungua kongamano la wadau wa michezo mapema hii leo Julai 26,2019 Mjini Mtwara.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza
akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kongamano la wadau wa michezo mkoani Mtwara (hawapo pichani) wakati Naibu Waziri huyo alipofungua kongamano la siku mbili mapema hii leo Julai 26,2019 mjini Mtwara.

Baadhi ya wajumbe wa kongamano la wadau wa michezo mkoani Mtwara
wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akifungua
kongamano la wadau wa michezo mapema hii leo Julai 26,2019 Mjini Mtwara.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia)
akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Evodi MManda wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akifungua kongamano la wadau wa michezo mapema hii leo Julai 26,2019 Mjini Mtwara.

***************

Na. WHUSM -Mtwara

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amewataka
maofisa Michezo kote nchini kusimamia michezo na sio kukaa maofisini wakisubiri
mashindano ya UMISHUMTA.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku mbili la wadau wa michezo mkoani Mtwara, Naibu Waziri Shonza ametoa rai kwa wajumbe kuhakikisha wanatumia siku hizo kwa kujadili changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo ya michezo.

“Ndugu washiriki, kutokana na umuhimu wa mafunzo haya ni vyema mtakapo
hitimisha muweke maazimio, Maafisa Michezo mpo hapa, hakikisheni maazimio ya
kongamano hili yanawasilishwa Idara ya Michezo kwa ajili ya kufanyiwa kazi,” Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara
(MTWAREFA), Edward Kapopo, amemuomba Naibu Waziri, Shonza kuwapatia maeneo kwa ajili ya kujenga vituo vya michezo ambavyo vitasaidia kukuza soka katika ukanda wa Kusini.

“Mheshimiwa Naibu Waziri, kituo cha Viva Soccer Academy kwa sasa tuna ofisi tu
hivyo tunalazimika kukodisha au kuomba maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za michezo,” alisema Bw.Kapopo.

Aidha, Naibu Waziri, Shonza ameiomba Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara kuona namna ya kukisaidia kituo hichbo kwa kuwapatia eneo litakaloendelezwa kwa ajili ya shughuli za michezo ili kuwa kitovu cha kuzalisha vipaji vya mpira wa miguu ukanda wa Kusini.

Kongamano hilo limewakutanisha maafisa michezo, viongozi wa vyama vya mpira wa miguu, walimu, waamuzi, wachezaji na waandishi wa habari za michezo ambapo watapata fursa ya mafunzo kwa wawezeshaji toka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na wadau mbalimbali wanaojishughulisha nampira wa miguu hapa nchini.