Home Mchanganyiko WAKAGUZI NA BODI YA UNUNUZI TANGULIZENI UZALENDO DKT.KIJAJI

WAKAGUZI NA BODI YA UNUNUZI TANGULIZENI UZALENDO DKT.KIJAJI

0

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji amewaagiza Wajumbe wa Bodi za Zabuni, Watendaji wa vitengo vya ununuzi, ukaguzi wa ndani na nje wa Taasisi za Serikali, kutanguliza uzalendo na uadilifu katika manunuzi ya umma, ili kusaidia Tanzania kufikia uchumi wa kati na uanzishwaji wa viwanda.

Akizungumza  jana Jijini hapa katika uzinduzi wa kongamano la saba la mwaka la Usimamizi wa umma lililoandaliwa  na Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma (PPRA),Dk.Ashatu alisema Serikali kwenye bajeti yake inatumia zaidi ya asilimia 75 katika manunuzi ya umma hivyo kila mtaalamu akizingatia  uadilifu Taifa litapiga hatua katika mipango
yake ya maendeleo.

“Eneo hili la manunuzi ni muhimu katika kutekelezwa miradi ya maendeleo, hivyo kila mtaalamu akiliheshimu na kutanguliza uzalendo na uadilifu taifa litafikia mipango yake yote iliyojipangia katika kufikia kiuchumi wa kati na uanzishwaji wa viwanda kabla ya mwaka
2025,”alisema.

Dk.Ashatu alipongeza PPRA kwa kufanya ukaguzi kwenye taasisi za umma na kuokoa fedha  zaidi ya Sh.bilioni 46 sawa na asilimia 23 ya taasisi zilizokaguliwa.

“Lakini lazima tujiulize kwanini tunasubiri kukaguliwa hiyo ni kukosa kulitendea haki taifa letu pia  tunakosa uzalendo,hivyo kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake  katika nafasi yake,”alisema.

Aidha aliagiza taasisi zote za umma kuhakikisha zinatumia mfumo wa kimtandao wa manunuzi (E Procurement) na hawatasita kuzifungia taasisi zisizotumia mfumo huo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo alisema kauli mbinu ya kongamano hilo ni:”Manunuzi katika miradi mikubwa kuelekea kiuchumi wa Viwanda.”

Alisema  uchumi wa viwanda utafikiwa endapo maafisa hao watazingatia sheria za manunuzi katika miradi mikubwa inayotekelezwa nchini.

Mhandisi Kapongo alisema PPRA ni muhimu katika kuisaidia Serikali kutimiza malengo,kwani katika ukaguzi waliofanya karibuni katika manunuzi  kwenye malipo ya Wakandarasi walibaini kufanywa malipo kinyume cha utaratibu na kuokoa  zaidi ya Sh.bilioni 46.

Alisema anaamini ukaguzi huo ungefanyika katika taasisi nyingi wangeokoa fedha zaidi ya hizo na kuwezesha Serikali kutimiza malengo yake.

Aliongeza kuwa wameshindwa kukagua taasisi zote za umma,kutokana na changamoto ya  ufinyu  wa bajeti na baadhi ya taasisi za umma kutoa ushirikiano  wakati wa ukaguzi.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Prof.Sufian Bukurura alisema Taasisi zao inauhaba wa Wafanyakazi kwani kwa sasa wapo 74 na mahitaji ni 152, hivyo aliomba Serikali kuwaongezea watumishi.

“Kwani tukiongezewa bajeti na wakaguzi itatusaidia kufanya ukaguzi zaidi ya Taasisi 100 tunazofanya sasa kati ya taasisi 540,mfano sasa tumekagua taasisi 100 nabtukaokoa zaidi ya Sh.bilionib46  je tungekagua zote zilizopo tungeokoa zaidi ya hizo,”alisema.