Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya Wizara yake. Kikao hicho kilifanyika Ukumbi wa Wizara jijini Dodoma, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimpa hati ya kiapo Afisa Utumishi wa Wizara hiyo, Andrew Kiangi, kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa Askari wa Majeshi hayo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, wakiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza katika kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya Wizara. Kikao hicho kilifanyika Ukumbi wa Wizara, jijini Dodoma, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuapisha Afisa Utumishi wa Wizara hiyo, Andrew Kiangi, kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa Askari wa Majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dodoma, leo. Kulia (aliyekaa) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.