Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Bashiru Ally,leo ametoa wito kwa wanachama wa chama hicho kuwapuuza wale watu wanaoendeleza mjadala usiokuwa na tija ndani ya chama hicho, na akawahakikishia kwamba chama hicho kiko imara.
Dk. Bashiru ameyasema hayo wakati akitoa pongezi kwa hatua ya wanaCCM Mkoa wa Dodoma, kutaka Kanali Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, makatibu wastaafu wa CCM kuchukuliwa hatua.
Hii ni baada ya makatibu hao wastaafu wiki iliyopita, kumwandikia barua Pius Msekwa, Katibu wa Baraza la Viongozi Wastaafu wa CCM wakilalamikia kuchafuliwa na Cryspian Musiba, anayejitambulisha kuwa mtetezi wa Rais John Magufuli.
Kwenye barua hiyo, Makamba na Kinana wamelalamika kuchafuliwa na kuzushiwa huku wakidai serikali imeshindwa kuchukua hatua. Hata hivyo,
wamehoji ‘ulinzi’ anaopewa Mtu huyo anayewachafua
wamehoji ‘ulinzi’ anaopewa Mtu huyo anayewachafua