Picha ikionyesha Muendesha mashine ya kuchanganya sege kutoka kampuni ya ukandarasi ya Booygues  ,  Dominic Heriman  akimuonyesha Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga jinsi wanavyochanganya sege kwa kutumia  komputa wakati katibu alipofanya ziara yake ya kukagua hatua iliofikia katika  ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 400 hapo  ni ndani ya store yard ya  Lot  T2  iliopo  katika kijiji cha Nanja .

Picha ikionyesha meneja wa mradi  kutoka kampuni ya Booygues Energies &services Potier Mathiew  akitoa maelekezo kwa  Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga pamoja na mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye pamoja na viongozi mbalimbali wa Tanesco wakiwemo wakandarasi wakati walipotembelea moja ya shimo lililopo tayari kwa ajili ya kusimamisha mnara.

Picha ikionyesha  Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akitoa maelekezo kwa mkandarasi

Picha ikionyesha  mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye akimfafanulia jambo  Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akitoa maelekezo kwa mkandarasi alipotembelea na ukagua ujenzi wa Lot T1 iliopo Nangwa  .

…………………..

Na Woinde Shizza ,Arusha

Serikali imesema imeridhishwa na kasi ya wakandarasi wanaojenga    Mradi  wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ,Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK  wa  kilovolti 400 inayopita katika mikoa ya  Singida Babati , Arusha hadi Namanga kwani  unaenda mbio na mpaka sasa  asilimia 51 ya ujenzi imeshakamilika .

 

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga wakati akihitimisha  ziara yake ya kukagua hatua iliofikia katika  ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 400 ambapo  ziara hiyo ilihusisha  kukagua njia ya umeme ya Namanga ,kituo cha kupoozea umeme cha Legur  kilichopo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Arumeru , pamoja na njia  za kusafirishia umeme zilizopo katika halmashauri ya Babati vijijini   katika kijiji cha Nagwa .

 

Alibainisha kuwa kazi zinazofanywa na wakandarasi waliopewa miradi hiyo  amerizishwa nazo sana na  kasi wanayoenda nayo kwani hadi sasa wameshafanya kazi kubwa na asilimia 51%  ya ujenzi wa mradi huo imekamilika  hivyo asilimia 49 %tu ndio zimebaki na anaamini wa kasi wakandasi hao wanayoenda nayo watakamilisha mradi huo kwa wakati  uliopangwa ambapo alisema kuwa  mradi huo unatakiwa kukamilika na kukabidhiwa rasmi kwa serikali mwezi  Aprili 2020 .

 

“nimepita nimeangalia hatua iliofikia mradi huu  wa njia ya usafirishaji wa umeme ambao miundombinu hii itaunganishwa katika vyanzo vya uzalishaji umeme ,kwa iyo miundombinu hii ni muhimu sana ,na nia ya ziara hii ni kuangalia tumefikia wapi hadi sasa hivi pia  kingine ni kuangalia kama kunachangamoto zozote zinazoikabili mradi ili kama zipo  serikali tuweze kuzitatua lakini tatu  kuangalia kama wakandarasi wanafanya kazi zao vizuri kwaiyo hayo ndiilikuwa sehemu kubwa ya lengo la ziara hii  sasa nimetembea nanapenda kusema nimerithishwa sana na utendaji  wa wakandarasi hawa kwani mapaka sasa hivi wameshasimamisha  minara zaidi ya mia moja kati ya minara  384 itakayo simamishwa sehemu zote  lakini pia misingi imeshawekwa kwa ajili ya ujenzi wa minara yote pia nimerizishw a kuona wakandarasi  wote wameshafika saiti   kulingana na Ratiba inavyosema”Alisema Luoga

 

Alisema katika mradi huu kuna Lot T5 ambayo ya kwanza inaanzia Singira mpaka Babati na Lot T2 ya pili inaanzia Singida hadi Arusha na Lot T3 ya tatu inaanzia Arusha mpaka Namanga ,Lot T4  inausisha ujenzi wa vituo vya kupooza umeme  ambapo kimoja kiko kisongo  na kingine  kitakuwepo pale Singida na Lot T5  itahusisha kusambaza umeme katika vijiji vyote  vinavyopitiwa na mradi  ,alisema kuwa kulingana na kasi ambayo wakandaras hawa wanaendanayo kunauwezekano mkubwa wa mradi huu kukamilika kabla ya ratiba iliyopangwa au utakamilika kwa wakati na mradi huu unahusisha ujenzi wa kilometa  400 kutokea Singida mpaka Namanga ,ambapo alibainisha kuwa serikali itahakikisha  vijiji vyote vinavyopitiwa na mradi huu vinapatiwa umeme  huku akisisitiza kuwa hakuna hata kijiji kimoja ambacho kitarukwa.

 

“ Sisi kama serikali tumewaagiza wakandarasi hawa wafanye kazi kila siku,wakandarasi wawatumie vijana wetu katika kazi zote kazi ambazo zinaitaji elimu na hata zile ambazo aziitaji elimu na katika swala hili napenda kuwapongeza wakandarasi  maana wametii maelekezo ya serikali na wameajiri vijana zaidi ya 400 ambao wanatoka katika vijiji ambavyo miradi imepita  kuanzia pale ulipoanzia Namanga hadi Singida ,pia tumewataka wakandarasi washirikiane najamii zinazozunguka miradi hii ili kusiwepo na changamoto  na katika hili tumewaambia wakiwahusisha wananchi katika swala la ulinzi wa miundo mbinu hii na hata katika zile  kazi ambazo zitaweza kuwapatia kipato hawa wananchi wetu ili wao wao wananchi waweze kuwa walinzi wa mradi huu ,pia  tumewaagiza wasimamie mradi uweze kukamilika katika viwango vinavyotakiwa ‘’Alisema Luoga

 Kwa upande wake mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye alisema kuwa aliwataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa wakandarasi hawa ikiwa ni pamoja na kuwasadia kazi mbalimbali za ujenzi ,lakini pia alisema serikali imewahaidi wakandarasi hawa  kuwasaida vitu mbalimbali  kwa wakati ikiwemo  kutoa vifaa vya ujenzi bandarini kwa wakati pamoja na kuwasaida vitu mbalimbali  ambavyo wakandarasi hao watakamwa ili tu wakamilishe mradi huo kwa wakati

 

Alisema kuwa kukamilika kwa miradi hii itasaidia kuchochea maendeleo ya vijijini na mijini pia itaongeza pato la nchi yetu kwani tutaweza kuingia katika sera ya uchumi wa viwanda na wawekezaji wataweza kuja kwa sababu watakuwa na uhakika wa uwepo wa umeme  lakini pia alitumia  mda huo kuwashukuru vingozi wanaotembelea mradi huo na kuangaia mwenendo wa kazi ,na maendeleo ya kaz i ,  waliahidi kufanya kazi kwa bidii kwa uhadilifu na kuhakikisha mradi unakamilika kwa muda ambao umepangwa na kwa fedha ambayo imepangwa kutumika ambapo alisema kuwa hadi kukamilika kwa mradi huu unatarajiwa kutumia dola za kimarekani milioni 258 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni  600