Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUHUSU HALI YA UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA KWA...

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU HALI YA UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA KWA MSIMU WA 2018/2019 NA UPATIKANAJI WAKE KWA MWAKA 2019/2020

0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu taarifa ya hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu wa
2018/2019 na upatikanaji wake kwa mwaka 2019/2020

Ndugu Wanahabari, 

Kila mwaka kati ya mwezi mei na juni, Wizara ya
Kilimo kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali hufanya tathmini ya hali ya
uzalishaji wa chakula na upatikanaji ili kujua;


i.
Hali
ya kiujumla ya uzalishaji wa mazao na upatikanaji wa chakula kwa Mikoa na
Halmashauri zote


ii.
Uzalishaji
wa mazao ya chakula na utekelezaji wa malengo ya uzalishaji hadi tarehe 31 Mei
kila mwaka.

  iii.
Athari
za visumbufu katika uzalishaji wa mazao

  iv.
Bei
ya mazao ya chakula na hali ya upatikanaji wa chakula sokoni katika Halmashauri
zote na kuainisha maeneo yenye dalili ya uhaba


v.
Hali
ya unyeshaji wa mvua na mwenendo wa uzalishaji wa mazao mashambani

Ndugu
Wanahabari

hali ya uzalishaji na upatikanaji wa mazao
ya chakula nchini imeendelea kuwa nzuri katika kipindi cha miaka mitano
mfululizo kufuatia uzalishaji wa ziada wa mazao ya chakula kuanzia msimu wa kilimo
wa 2013/2014 hadi 2017/2018 ambapo kwa msimu wa 2018/2019 nchi imejitosheleza ikilinganishwa
na mahitaji.

Ndugu Wanahabari, 

katika kufanya tathmini ya hali ya
chakula, hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula na usalama wa chakula tunaangalia
baadhi ya mazao muhimu yanayohitajika zaidi kama vile mahindi, mtama na ulezi,
mchele, mikunde, ngano, ndizi, muhogo na viazi.

Ndugu
Wanahabari,
 

katika kipindi hicho, nchi imekuwa na
kiwango cha utoshelevu kati ya asilimia 120 hadi 125 na imekuwa ikizalisha
ziada kati ya tani 2,582,717 hadi 3,322,689. Mafanikio hayo yanatokana na
sababu mbalimbali ikiwemo hali ya hewa nzuri, pamoja na usimamizi na
utekelezaji mzuri wa sera na mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali
pamoja na Wadau wengine wa masuala ya kilimo ili kuongeza tija na uzalishaji.

Ndugu Wanahabari, 

Wizara
ya Kilimo mwezi Mei hadi Juni 2019 ilifanya Tathmini ya Hali ya Uzalishaji wa Mazao
ya Chakula kwa msimu wa 2018/2019 na Upatikanaji wa Chakula kwa  mwaka 2019/2020 katika mikoa yote 26 Tanzania
Bara kwa lengo kubaini uzalishaji na mahitaji.

Ndugu
Wanahabari, 

Matokeo yanaonesha kuwa hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kitaifa katika msimu wa 2018/2019 utafikia tani 16,408,309
kwa mlinganisho wa nafaka (Grain Equivalent) ambapo nafaka ni tani
9,007,909 na siyo nafaka tani 7,400,400.

Ndugu
Wanahabari, 

Ikilinganishwa
na msimu uliopita, uzalishaji wa mazao ya chakula umeshuka kwa tani
483,665
ambapo nafaka hususan mahindi
yameshuka kwa tani 455,642 na mchele kwa tani 210,454. Aidha, uzalishaji
wa siyonafaka (non cereals) umeongezeka kwa tani 46,283.

Ndugu
Wanahabari, 

uzalishaji wa mazao ya nafaka ulifikia asilimia 103
na mazao yasiyo ya nafaka yalifikia asilimia 145. Hivyo, uzalishaji wa jumla wa
mazao ya nafaka na yasiyo ya nafaka ulifikia asilimi 119.

Ndugu
Wanahabari,
 

Aidha mchango wa uzalishaji wa mazao ya chakula
kitaifa katika msimu wa 2018/2019 unaonesha kuwa mahindi yamechangia kwa
asilimia 35, muhogo kwa asilimia 17, mchele kwa asilimia 12, viazi kwa asilimia
10 na mazao mengine.

Ndugu
Wanahabari,
 

Pamoja
na hali hiyo,
utengamano wa usalama wa chakula unatarajiwa kuwa wa
viwango tofauti kimkoa. Aidha, hali ya uwepo na upatikanaji wa chakula kwa sasa
ni nzuri kutokana na uzalishaji mzuri wa msimu wa 2017/2018.

Ndugu
Wanahabari

Kwa
kuzingatia Kigezo cha Upimaji wa Kiwango cha Utoshelevu (Self Sufficiency Ratio – SSR), matokeo yanaonesha kuwa kwa mwaka wa
chakula 2019/2020, nchi itakuwa na kiwango cha Utoshelevu cha asilimia 119.

Ndugu
Wanahabari

Tathmini
imeonesha, h
ali ya chakula inatarajiwa kuwa ya kiwango cha Ziada kwenye mikoa 11 ya Rukwa, Ruvuma, Songwe,
Katavi, Njombe, Mbeya, Kigoma, Iringa, Kagera, Morogoro, na Mtwara kwa asilimia
128 hadi 227. Aidha, kutakuwa na hali ya Utoshelevu  kwenye mikoa 7 ya Geita, Simiyu, Pwani, Lindi,
Manyara, Singida na Tanga kwa asilimia 109 hadi 119 na Upungufu kwenye mikoa 8 ya Dodoma,
Mara, Mwanza, Arusha, Tabora, Shinyanga na Kilimanjaro kwa asilimia kati
ya  98 hadi 99.

Ndugu
Wanahabari

Mkoa
Dar es Salaam si miongoni mwa mikoa ya uzalishaji wa mazao na hivyo
kujitosheleza kwa asilimia 3 tu kutokana na eneo dogo linalolimwa lisilokidhi
mahitaji ya chakula ya wakaazi wake. Ingawa mkoa huu unawekwa kwenye upungufu
wa chakula kwa maana ya uzalishaji katika mashamba, mkoa huu una vyakula vingi
vinavyoingia sokoni kutoka katika mikoa 25 ya Tanzania bara na hivyo kuwa na
Utoshelevu kwa vipindi vyote.  

Ndugu
Wanahabari

Tathmini imebainisha kuwa
uwepo wa maeneo (pockets)
yenye dalili za upungufu wa chakula kwenye Halmashauri 46 katika mikoa 13 kama ifuatavyo;

·      Mkoa wa
Dodoma katika Halmashauri 7 za Bahi, Chamwino, Chemba, Kondoa, Kongwa na
Mpwapwa;

·   Mkoa wa
Mara katika Halmashauri 5 za Bunda DC, Bunda TC, Musoma DC, Musoma MC na Rorya;

·     Mkoa wa
Tabora katika Halmashauri 5 za Uyuyi, Igunga, Nzega DC, Nzega TC na Kaliua;

·   Mkoa wa
Shinyanga katika Halmashauri 4 za Kishapu, Shinyanga DC, Shinyanga MC na
Msalala;

·     Mkoa wa
Kilimanjaro katika Halmashauri 4 za Mwanga, Same, Siha na Hai,

·  Mkoa wa
Mwaza katika Halmashauri 4 za Misungwi, Ukerewe, Kwimba na Sengerema;

·       Mkoa wa
Manyara katika Halmashauri 4 za Simanjiro, Kiteto, Hanang na Mbulu TC;

·
Mkoa wa
Simiyu katika Halamshauri 4 za Itilima, Maswa, Meatu na Busega;

·
Mkoa wa
Arusha katika Halamshauri 3 za Longido, Ngorongoro na Monduli;

·
Mkoa wa
Singida katika Halmashauri 3 za Ikungi, Manyoni na Singida DC;

·
Mkoa wa
Tanga katika Halmshauri 1 ya Tanga jiji;

·
Mkoa wa
Lindi katika Halmashauri 1 ya Lindi DC na

·
Mkoa wa
Iringa katika Halmashauri 1 ya Iringa DC.

Ndugu
Wanahabari

Msimu
wa uzalishaji wa 2018/2019 ulikabiliwa na changamoto mbalimbali katika baadhi
ya maeneo zilizoathiri uzalishaji wa mazao kwa viwango tofauti na kusababisha
kushuka kwa uzalishaji wa mazao hususan zao la mahindi. Miongoni mwa changamoto
hizo ni pamoja na:-

(i)
Katika maeneo yanayopata mvua
misimu miwili (Bimodal Areas) mvua za
vuli katika maeneo mengi hazikufanya vizuri. Aidha, mvua za masika zilichelewa
sana kuanza na hivyo kuathiri shughuli za kilimo katika maeneo hayo,

(ii)
Kuchelewa kuanza kunyesha kwa
mvua na mtawanyiko usioridhisha kwenye baadhi ya maeneo ya nchi yanayopata mvua
msimu mmoja (Unimodal Areas) hususan
katika mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, na baadhi ya maeneo ya
mikoa ya Morogoro, Mwanza, Mara, Simiyu na Manyara,

(iii)
Visumbufu hususan viwavijeshi
vamizi (Fall Army Worm – FAW), panya
na Kweleakwelea.

Ndugu
Wanahabari

Kufuatia
matokeo ya Tathmini hii,
Serikali
inachukua / itachukua hatua zifuatazo;

·
Kuimarisha
Mfumo wa ukusanyaji taarifa za usalama wa chakula nchini ili kuweza kuchukua
hatua stahiki pindi inapobidi,

·
Kufanya
Tathmini ya Kina ya Hali ya Chakula na Lishe mapema katika Halmashauri
zilizobainika kuwa na maeneo yenye viashiria vinavyoweza kusababisha upungufu
wa chakula,

·
Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko
wanatarajia kuanza ununuzi wa mazao ya chakula kutoka kwenye maeneo yenye
ziada,

·
Kuimarisha
mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo viuatilifu,
mbegu na mbolea.

·
TRA
pamoja na Wataalam wa kilimo katika vituo vya mipaka ya nchi  kusimamia kikamilifu usafirishaji wa mazao
yanayokwenda nje ya nchi ili kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi za kiasi
kinachosafirishwa nje ya nchi.