Moja ya nyumba zilizowashwa umeme na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu katika kijiji cha Mkindo Wilayani Kaliua mkoani Tabora.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( mwenye kilemba) alizungumza na vijana wanaofanya kazi ya useremala kwa kutumia umeme wa jua katika kijiji cha Mgambo wilayani Sikonge, Naibu Waziri alifika kijijini hapo kutembelea kampuni ya uwekezaji inayozalisha umeme jua na kuwauzia wananchi.
Wakazi wa kijiji cha Wema mwenye ulemvu wakikabidhiwa kifaa cha umeme tayari ( UMETA) kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati , Subira Mgalu, aliyekuwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini wilayani Sikonge, mkoani Tabora.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( katikati) akipata maeneo ya namna ya mtambo wa kuzalisha umeme jua unavyofanya kazi katika kijiji cha Mgambo, Mkola na Mwenge wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Naibu Waziri Subira Mgalu( mwenye kilemba) na viongozi wengine wakikata utepe kuashirika kuwasha umeme katika moja ya taasisi za dini katika kijiji cha Mkindo wilayani Kaliua, mkoani Tabora.
Ujenzi ukiendelea katika kituo cha kupokea na kupoza umeme katika kijiji cha Uhuru, wilayani Urambo mkoani Tabora.
…………………..
Na Zuena Msuya, Tabora
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema mameneja wa Shirika la Umeme nchini, (Tanesco) waongeze idadi ya wateja kwa kuwaunganishia huduma ya umeme wananchi waliopo vijijini kwa bei ya shilingi 27,000.
Hatua hiyo ni kigezo cha kupima utendaji kazi wa mameneja hayo katika Kanda,Mikoa pamoja na Wilaya mbalimbali nchini.
Mgalu alisema hayo kwa nyakati tofauti, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa Umeme Vijijini,( REA) katika Wilaya za Ulyankhulu, Kaliua, Urambo pamoja na Sikonge Mkoani Tabora, Julai 18,2019.
Katika Wilaya hizo, Mgalu aliwasha Umeme katika makazi ya watu, Nyumba za ibada,taasisi za umma, visima vya maji pamoja na kuzungumza na wananchi wa eneo hayo.
Akiwa katika wilaya hizo, Mgalu aliwasha umeme katika kijiji cha Limbula na Kasunga wilayani ni Kaliua, vilevile katika kijiji cha Mfindo wilayani Ulyankhulu.
Aidha akiwa katika wilaya Urambo aliwasha umeme katika kijiji cha Wema, pia aliwsha umeme katika kijiji Kikungu wilayani Sikonge na kuzungumza na wananchi.
Alisema Mameneja wa maeneo husika ndiyo wenye dhamana kubwa ya kuwafuata wateja katika makazi na kuwashawishi kuunganishwa na Umeme badala ya kukaa Ofisini na kusubiri wateja.
“Mradi wa REA umekwisha viunganisha na kuwasha umeme katika vijiji vingi vya Wilaya mbalimbali, naawaagiza mameneja kufanya kazi ya kuwafuata wananchi huko walipo mkawape elimu ili muwaunganishe na Umeme, kwa bei ya shilingi 27,000, tunataka kuona idadi ya watumiaji Umeme inaongezeka”, Alisema Mgalu.
Tangu mradi wa REA umeanza tayari zaidi ya wateja laki tisa(900,000) wameungamishwa na umeme na bado zoezi hilo linaendelea.
Katika ziara yake hiyo, Mgalu alikagua ujenzi wa kituo cha kupokea na kuponza umeme kilichopo katika kijiji cha Uhuru wilayani Urambo ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho inayoendelea.
Sambamba na hilo, alikagua eneo ambalo litajengwa kituo kingine cha kupokea na kupoza umeme katika kijiji cha Ipole wilayani Sikonge, ambacho kinatarajia kuanza kujengwa hivi karibuni.
Vituo hivyo vinajengwa mahsusi kwa lengo la kuimarisha upatikani wa umeme mwing na wakutosha katika Mikoa ya Tabora, Kigoma na pamoja na Katavi,pia mikoa hiyo nayo iunganishwe na gridi ya taifa, na kuacha kutumia umeme unaotokana na mafuta mazito.
Katika hatua nyingine alitembelea kagua kampuni ya Power Corner katika kijiji cha mgambo wilayani Sikonge, inayofanya kazi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya jua na kuwauzia wakazi wa kijiji cha Mgambo, Mwenge pamoja na Mkola.
Kituo hicho kilipata zabuni ya zaidi ya shilingi milioni 500 kutoka kwa Wakala wa Nishati Vijiji (REA) kwa lengo la kuchangia utekelezaji wa kituo hicho ikiwa ni kutekeleza azma ya serikali kuwainua wazalishaji wadogo wa umeme.
Naibu waziri aliwaagiza watendaji wa kituo hicho kutoa huduma bora zinazoendana na ghara wanazolipia wananchi ili mradi huo uwanufaishe wananchi na si kuwakandamiza.