KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Dkt.BASHIRU ALLI amelitaka Shirikisho la Umoja wa wamachinga nchini Taifa (SHIUMA)kuzingatia mshikamano miongoni mwao ili kukabili migogoro ya kiuongozi inayoweza kutokea.
Ushauri huo ni miongoni mwa mambo matatu aliyotoa kwao baada ya SHIUMA kufika ofisini kwake jijini Dodoma kuwasilisha pongezi zao kwa Mweyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)dokta JOHN MAGUFULI kwa juhudi zake anazofanya za kuwatambua shughuli wanazofanya.
Akipongea pongezi hizo kwa niaba ya Rais dokta MAGUFULI,dokta BASHIRU amesema pia wanapaswa kuwekeza kwenye elimu na kutumia jasho na nguvu zao katika kuwalea watoto kwenye maadili.
Wakizungumza na waandishi wa Habari Makao makuu CCM Taifa,viongozi wa shirikisho hilo wamesema lengo kubwa la kufika kwao ni kumpongeza Rais MAGUFULI kwa hatua yake ya kuwapa viitambulisho vinavyowasaidia kufanya shughuli zao bila ya bugudha.
Aidha,Mwenyekiti wa Machinga Taifa Bw.Matondo Masanja amesema wazo La vitambulisho vya machinga ni la machinga wenyewe hivyo wanasiasa wanapaswa kuacha kuupotosha umma kuwa ni la Rais Magufuli bali yeye alipokea mawazo ya machinga hao la kuwapatia vitambulisho na kulitekeleza mara moja ilikuwaondolea kero mbalimbali.
SHIUMA kwa sasa ina wanachama katika mikoa 16 ya tanznaia Bara lengo lake likiwa ni kufika katika mikoa yote nchini.