Wananchi wakipata huduma katika banda Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA
Mkuu wa Kitengo wa Huduma za Bidhaa za Mawasiliano wa TCRA, Thadayo Ringo akizungumza na wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada wilayani Bukoba.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) Thomas William akizungumza na wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA wilayani Bukoba.
Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akizungumza katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada kwa kushirikiana na wadau Wilayani Bukoba mkoani Kagera.
*************
Wakazi wa Bukoba mkoani Kagera na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Meneja wa Kanda ya Ziwa wa TCRA Francis Mihayo amesema ni fursa kwa wananchi wa Bukoba kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano.
Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano.
Mihayo amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
“TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo”amesema Mihayo