Home Mchanganyiko BENKI YA CRDB YATOA MILIONI 150 KUDHAMINI MKUTANO MKUU WA ALAT 2019

BENKI YA CRDB YATOA MILIONI 150 KUDHAMINI MKUTANO MKUU WA ALAT 2019

0

Mkurugenzi wa Wateja wa Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB –Boma Labala (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 150 kwa ajili ya audhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT – 2019 kwa Mwenyekiti wa ALAT taifa Mheshimiwa Gulamhafeez Mukadam. Kushoto ni Maneja Mwandamizi waBiashara za  Serikali za Mitaa wa Benki ya CRDB Suzana Shuma na kulia ni Mheshimiwa Zainab Vullu, Muwakilishi wa Wabunge ALAT.

Mwenyekiti wa ALAT taifa Mheshimiwa Gulamhafeez Mukadam akizungumza katika makabidhiano hayo.

………………..

Benki ya CRDB imekabidhi hundi ya mfano ya shilingi Milioni 150 kwa uongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kwaajili ya udhamini wa mkutano mkuu wa 35 wa ALAT taifa unaotarajia kufanyika kuanzia tarehe 22 jJulai hadi 24 jijini Mwanza.

Fedha hizo ni kwa ajili ya kugharamia gharama za mkutano mkuu unaotarajia kukutanisha wajumbe zaidi ya 500 kati yao wakiwa mameya, kutoka halmashauri zote nchini, wakurugenzi wa halmashauri wapatao 185, wawakilishi wa mikoa na wizara mbalimbali ambao jumla yao wanafika zaidi ya 500.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Goldcrest jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Boma Labala alisema kuwa Benki ya CRDB inathamini sana mchango wa Serikali za mitaa hususan halmashauri katika ustawi wa uchumi na maendeleo ya Taifa. “Benki ya CRDB inatambua umuhimu wa ALAT katika kuchochea maendeleo ya taifa letu, pasi na shaka hiki ni chombo kinachounganisha pamoja mamlaka na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya Serikali za Mitaa hapa nchini ambapo ndio hasa wanamgusa Mtanzania katika ngazi ya chini. Hii ndio sababu kubwa iliyotufanya sisi kuwa tayari kushiriki mkutano huu, kwa kuamini kuwa mikakati na maazimio yanayofikiwa hapa leo yatakwenda kuongeza kasi maendeleo ya taifa letu na kuwagusa watanzania walio wengi”.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulamhefeez Mukadam alisema kuwa taasisi yao inathamini sana udhamini huo wa Benki ya CRDB kwani kwa kiasi kikubwa utachangia gharama za uendeshaji wa mkutano huo muhimu. Mheshimiwa Mukadam alisema kuwa Benki ya CRDB imekuwa mdau mkubwa wa Serikali za mitaa kwa kuendelea kutoa huduma za kifedha kwa halmashauri zaidi ya 60 nchini na mikopo kwa halmashauri hizo na wafanyakazi wake. “CRDB ni mdau wetu muhimu sana na tunashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono” alisema.