Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth
Magandi (kulia) akizungumza na viongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar
ambao leo wametembelea Hospitali ya Mloganzila kwa lengo la kujifunza
muonekano na upangaji wa huduma katika hospitali za kisasa. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mnazi Mmoja Dkt. Abdulwakil Idrisa
Abdulwakil.Viongozi wa Hospitali ya Mmnazi Mmoja Zanzibar wakiwa katika
mkutano kabla ya kuanza kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali.
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi MNH- Mloganzila Mhandisi Andrew
Fungamali (katikati) akielezea kuhusu mfumo wa maji na mfumo wa kuzima moto
unavyofanya kazi.
Kiongozi kutoka kitengo cha usafishaji damu MNH-Mloganzila
Nurdin Mtumbuka (aliyesimama katikati) akiwaeleza viongozi wa Hospitali ya
Mmnazi Mmoja kuhusu utoaji wa huduma ambapo kitengo hicho kina uwezo wa
kuhudumia wagonjwa 36 kwa siku.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Redemptha Matindi
(aliyesimama katikati) akizungumzia huduma zinazopatikana katika wodi ya
wagonjwa mashuhuri katika Hospitali ya Mloganzila.Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Mloganzila na Mmnazi Mmoja
Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea
maeneo mbalimbali ya hospitali hii leo.
*******************
Wajumbe wa Bodi Zanzibar waipongeza Mloganzila
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila- imewekea mikakati mbalimbali ya
kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwemo
huduma za kibingwa na kibobezi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa
Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi wakati akizungumza na viongozi wa
Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar ambao wamefanya ziara ya siku moja katika
Hospitali ya Mloganzila kwa lengo la kujifunza muonekano na upangaji wa
huduma katika hospitali za kisasa.
Ujumbe wa viongozi hao umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa
Hospitali hiyo Dkt. Abdulwakil Idrisa Abdulwakil.
Dkt. Magandi amesema dhamira ya hospitali ni kuwawezesha wananchi wengi
kupata huduma za kibingwa sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali za
kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Pia amesema idadi ya wagonjwa katika Hospitali ya Mloganzila inaendelea
kuongezeka ambapo katika kipindi cha Oktoba mwaka jana wagonjwa wa nje
walikua takribani 200 kwa siku lakini kwa sasa wanafikia wagonjwa 500 kwa siku
huku wagonjwa wa ndani wakiongezeka kutoka 100 mpaka zaidi ya 300.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Mnazi
Mmoja Dkt. Abdulwakil Idrisa Abdulwakil ameshukuru ushirikiano uliopo na
kueleza kuwa Hospitali ya Mloganzila na Mnazi Mmoja wamekuwa na ushirikiano
wa karibu wa kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ikiwemo huduma
ya kusafisha damu na huduma ya mama na mtoto.