Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kasism Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Katibu na Meneja wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga kuhusu pamba iliyokusanywa na wakulima kwenye ghala la ushirika huo, Julai 15, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mikokoteni iliyosheheni pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga alikofanya ziara ya siku moja ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Wananchi wa kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba, Julai 15, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)