Home Mchanganyiko RAIS MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZA POLISI

RAIS MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZA POLISI

0

*****************

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewaomba wananchi wa
mkoa wa Geita pamoja na maeneo jirani na mkoa huo kujitokeza kwa wingi
siku ya jumatatu kwenye tukio la uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari,
uzinduzi utakaofanyika katika eneo la magogo mkoani humo.

IGP Sirro amesema kuwa, katika tukio hilo ambalo litaongozwa na Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, ambapo atazindua
zaidi ya nyumba 114 zilizokwisha kamilika huku matarajio ya mradi huo ni
kuwa na nyumba takribani 400 kwa nchi nzima.

Aidha, IGP Sirro amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na
Jeshi la Polisi katika kuhakikisha askari wanaishi kwenye mazingira mazuri
jambo ambalo litachangia weledi na uwajibikaji hususan kulinda maisha ya raia
na mali zao.