Home Burudani BENSON WA HAUZIMI AVUNJA UKIMYA KATI YAKE NA ROSE NDAUKA

BENSON WA HAUZIMI AVUNJA UKIMYA KATI YAKE NA ROSE NDAUKA

0

******************

NA EMMANUEL MBATILO

MSANII wa kizazi kipya hapa nchini, Benson William maalufu Benson wa Hauzimi ameamua kuweka wazi uhusiano wake kati yake na msanii wa filamu hapa nchini Rose Ndauka baada ya taarifa nyingi kuzagaa mitandao na kila sehemu yakuwa hao wawili wapo katika mahusiano ya kimapenzi.

Akizungumza na Fullshangwe blog hivi karibuni, Benson alisema kuwa uhusiano wake na msanii huyo ni katika kazi kwani mwanzo alikuwa hana menejimenti ya kumsimamia katika kazi zake hivyo kwasasa amepata menejimenti ambayo inasimamiwa na Rose ndauka.

“Rose amekuwa mtu wangu wa karibu sana katika kazi kwani amekuwa akinisaidia hasa kutokana na mwanzo sikuwa na menejimenti ya kunisimamia lakini kwasasa namshukuru mungu na tunaenda vizuri na ninategemea makubwa hivyo mashabiki wasubiri mambo mazuri”.Alisema Benson.

Benson kwasasa ameachia wimbo wake unaokwenda kwa jina la Mashallah ambao mpaka sasa unaendelea kufanya vizuri.