Home Mchanganyiko NANE NANE KUANZA TAREHE 28 MWEZI HUU MKOANI SIMIYU

NANE NANE KUANZA TAREHE 28 MWEZI HUU MKOANI SIMIYU

0

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw.Jumanne Sagini akiongea na wanahabari katika Maonesho ya biashara katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

NA EMMANUEL MBATILO

*************

Maonesho ya bidhaa za Wakulima kuelekea Siku kuu ya wakulima duniani inatarajiwa kuanza tarehe 28 mwezi huu mwenyeji akiwa ni Simiyu ambaye pia nia mwaandaaji wa maonesho hayo.

Maonesho hayo yatafanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Wilaya ya Bariadi Mjini mkoa wa Simiyu baada ya kuwa mwenyeji na muandaaji wa maonesho hayo.

Ameyasema hayo leo Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw.Jumanne Sagini katika Maonesho ya biashara katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

“Nawasihi wananchi kwaujumla waweze kujitokeza na kutumia fursa hii kwa kufika na kuonesha shughuli za zao za kilimo pamoja na Uvuvi katika maonesho hayo”. Amesema Bw.Sagini.

amesema kuwa kutakuwa na mazingira mazuri ambayo yatamrahishia mteja au mtu ambaye amefika pale kwaajili ya maonesho kufurahia kwani barabara na majengo ya maonesho yamekarabatiwa na kuhakikisha usalama kwa ambao watafika.