Home Mchanganyiko IGP SIRRO AKEMEA VITENDO VYA RUSHWA

IGP SIRRO AKEMEA VITENDO VYA RUSHWA

0

***************

12/07/2019 MUSOMA, MARA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka askari wa Jeshi hilo
kote nchini kujiepusha na vitendo vya rushwa, utovu wa nidhamu na badala
yake kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

IGP Sirro amesema hayo akiwa mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ambapo
alisema kuwa, Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi wameendelea kuufanya mkoa huo kuwa katika hali ya usalama.

Aidha, IGP Sirro akiwa hapa mkoani Mara, amefanya ukaguzi wa mradi wa
nyumba za makazi ya askari ambapo hadi kufikia sasa maendeleo ya mradi huo
yamefikia hatua ya kukamilika kwa nchi nzima huku Mhe.Rais Dkt. John
Magufuli akitarijiwa kuzindua nyumba 114 zilizojengwa huku matarajio ya
ujenzi huo ni kuwa na jumla ya nyumba 400 nchi nzima.