Home Mchanganyiko Unesco kuendesha mafunzo kwa radio 25

Unesco kuendesha mafunzo kwa radio 25

0

******************

 Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) litaendesha mafunzo kwa vituo vya radio 25 nchini Zanzibar kuanzia leo hadi Julai 18 mwaka huu.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha waandishi wa habari wa radio na watangazaji kutengeneza vipindi vya maendeleo huku vikizingatia jinsi.

 UNESCO itawajengea uwezo waandishi wa habari kuwa na uwezo wa kutengeneza taarifa za habari zenye uhusiano na maendeleo na jinsi.

Aidha radio zote zinazoshiriki zitapatiwa kiasi cha fedha kutumika katika kuboresha uzalishaji wa vipindi na taarifa za habari kwa kuzingatia jinsi na maendeleo kwa muda wa miezi sita.

Lengo kuu la kuboresha vipindi hivyo ni kuwezesha zaidi sauti za wanawake kusikika kupitia vipindi mbalimbali vya mahojiano.

UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswisi linaendesha mradi wa kuwezesha radio za wananchi kuwa na  mifumo ya tehama inayosaidia kutengeneza vipindi vizuri na vyenye kuwezesha maendeleo endelevu nchini.