Home Mchanganyiko Rais Dkt. Magufuli Azindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato

Rais Dkt. Magufuli Azindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiimba wimbo wa Taifa wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato leo Mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi Usu wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato leo Mkoani Geita.-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato leo Mkoani Geita ambapo alieleza mipango ya Serikali ya kuendelea kukuza na Kuendeleza Sekta ya Utalii nichini

-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha Tuzo ya Serengeti Kuwa Hifadhi Bora Afrika baada ya Kukabidhiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato leo Mkoani Geita.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akiongea wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato leo Mkoani Geita ambapo alisema katika. Ikakati ya Wizard hiyo kuendeleza sekta ya Utalii, wameanzisha shughuli mbalimbali zinazoambatana na utalii ikiwemo kuanzisha utalii wa fukwe katika Ziwa Victoria.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akimpa Zawadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya Sanamu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato leo Mkoani Geita.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwavisha vyeo vya Kuwa Makamishna wakuu wa Taasisi nne za TAWA, TANAPA, TFS na Mamlaka ya Ngorongoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali baada ya kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato leo Mkoani Geita.