Home Mchanganyiko IGP SIRRO AKAGUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI...

IGP SIRRO AKAGUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI POLISI.

0

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (aliyesimama), akizungumza na baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza, wakati
alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo ambapo pia alitembelea mradi wa
ujenzi wa nyumba za makazi ya askari zinazojengwa katika eneo la
Nyamhongoro. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akikagua gwaride aliloandaliwa kwa
ajili yake wakati alipowasili mkoa wa Mwanza kwa ziara ya kikazi ambapo pia
alitembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya askari zinazojengwa
katika eneo la Nyamhongoro. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia), akizungumza na baadhi ya
wananchi aliokutana nao katika kivuko eneo la Busisi mkoani Mwanza, wakati
akiwa safarini kuelekea mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi, mbele yake ni
kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro. Picha na Jeshi la Polisi.