Home Teknolojia WALIMU WATUMIE VIFAA HALISI KUWAFUNDISHA WANAFUNZI KWA VITENDO-MHANDISI ENELISA

WALIMU WATUMIE VIFAA HALISI KUWAFUNDISHA WANAFUNZI KWA VITENDO-MHANDISI ENELISA

0

Baadhi ya vifaa vya kufundishia( Teaching Modals) ambavyo vimebuniwa na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro(Morogoro Vocational Teacher’s Traning College)

Mkufunzi wa Chuo cha Ualimu wa ufundi stadi Morogoro (Morogoro Vocational Teacher’s Traning College), Mhandisi Enelisa Andengulile akiongea na mtaje ambaye ameweza kufika katika ofisi za Chuo hicho katika Maonesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

************

NA EMMANUEL MBATILO

Walimu watakiwa kutumia vifaa vitakavyomrahisishia mwalimu huyo kufundishia hasa kwenye suala la  vitendo kwa wanafunzi ili kuweza kupata uelewa mkubwa kuendana na uhalisia.

Ameyasema hayo leo Mkufunzi wa Chuo cha Ualimu wa ufundi stadi Morogoro (Morogoro Vocational Teacher’s Traning College), Mhandisi Enelisa Andengulile  katika Maonesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Fullshangwe blog, Mhandisi Enelisa amesema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakipata wakati mgumu kuelewa kitu ambacho anafundishwa hasa pale anapofikilia kwa kina hicho anachofundishwa lakini mwalimu akitumia kifaa maalumu cha kufundishia kwa vitendo kitamsaidia mwanafunzi kuelewa hicho kitu ambacho anafundishwa.

Mhandisi Enelisa amesema kuwa wao kama chuo cha walimu wa ufundi Stadi, vifaa vya kufundishia kwa vitendo wamevipa kipaumbele kwani wanahitaji kupata walimu ambao wataweza kufundisha vizuri wanafunzi ili kuweza kukuza viwanda nchini kuendana na kauri ya Serikali ya awamu ya Tano yakufikia Uchumi wa kati hasa katika sekta ya viwanda.

Amefafanua kuwa  chuo hicho ni pekee nchini Tanzania ambacho kinatoa kozi za ualimu wa ufundi stadi ambapo wanapokea wanafunzi wa kada mbalimbali na kisha kuwaandaa kuwa walimu mahiri ambao watakwenda kufundisha vyuo vya ufundi stadi katika maeneo yote nchini.

“Chuo hiki ni chuo pekee Afrika Mashariki kinachotoa kozi za Ualimu wa Ufundi Stadi hivyo tunapokea wanafunzi waliomaliza kidato cha nne wenye ufahuru wa angalau pass nne na awe amesoma chuo chochote cha Ufundi na kupata cheti awali au diploma”. Amesema Mhandisi Enelisa.