Home Teknolojia TEKNOLOJIA YA KAMERA ZA ULINZI HUSAIDIA KUOKOA AJIRA KWA VIJANA WANAOMALIZA MAFUNZO...

TEKNOLOJIA YA KAMERA ZA ULINZI HUSAIDIA KUOKOA AJIRA KWA VIJANA WANAOMALIZA MAFUNZO (VETA)

0

Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Kipawa ICT, Bw.Stanley Masanja akiongea na mmoja wa wateja waliofika katika maonesho ya biashara yanayoendelea  katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

*************

NA EMMANUEL MBATILO

Wanafunzi wa udereva wamekuwa wakimaliza kwa wingi lakini ajira kwao inmekuwa changamoto hivyo Chuo cha Ufundi VETA Kipawa ICT kimeamua kuwaletea Udereva wa Teknolojia ambao utamsaidia mwanafunzi kujiajili na kupewa msaada wa kutosha kutoka VETA.

Ameyasema hayo leo Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Kipawa ICT, Bw.Stanley Masanja katika maonesho ya biashara yanayoendelea  katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

“Tumeona huyu mwanafunzi anavyomaliza asitegemee kwenda tu kuajiliwa badala yake anaweza kufanya kazi nyingine ambazo sisi tumeziongeza na kazi moja wapo ni kupachika kamera katika magari ambazo faida yake ni pamoja na usalama kwenye gari lako lakini pia zinarahisisha mashambani”. Amesema Bw. Masanja.

Amesema mwanafunzi asiweze kusubiri kuajili bali afunguo ofisi na kujitangaza yakuwa anauwezo wa kufunga kamera za kwenye gari na hivyo akipata wateja kadhaa anaweza fika VETA na kujielezea na atapewa kamera kwa bei nzuri na kupata faida kwake na kwao pia.

“Kamera hizi pia zinafaida kwa wakulima kwani humsaidia pindi pale mkuma akiwa analima kamera hizo hufunga katika jembe la kulimia  na kuangali wapi anakosea na kurekebisha kuliko kumaliza kulima na kutafakari ni wapi umekosea hivyo kamera ni muhimu inaweza kumsaidia”. Ameongeza Bw.Masanja.