Home Mchanganyiko RC MAKONDA AITAKA OFISI ILIYOTUMIA VIBAYA PESA ZILIZOCHANGWA KWAAJILI YA WACHEZAJI TAIFA...

RC MAKONDA AITAKA OFISI ILIYOTUMIA VIBAYA PESA ZILIZOCHANGWA KWAAJILI YA WACHEZAJI TAIFA STARS KUZIREJESHA MARA MOJA

0

***************

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamti ya kusaidia Ushindi kwa timu ya Taifa stars Mhe. Paul Makonda ameitaka Ofisi iliyochangisha fedha kwaajili ya Timu ya Taifa Stars na kutumia fedha hizo kwa matumizi binafsi kuhakikisha wanazirejesha fedha hizo na kuziingiza kwenye akaunti ya Baraza la Michezo Tanzania BMT na akaunti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF mara moja.

RC Makonda amesema Ofisi hiyo ilichangisha mamilioni ya fedha kutoka kwa makampuni, Bank na wadau wa michezo lakini cha kushangaza ofisi hiyo ilitumia pesa hizo kwenda na watu nchini Misri Kulala hotelini na kufanya utalii jambo ambalo ni kinyume na lengo.

Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo leo Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kuwapokea Wachezaji wa Timu ya Taifa Stars na viongozi wa timu wakitokea kwenye michuano ya AFCON 2019 Nchini Misri ambapo amewapongeza wachezaji hao kwa kujituma uwanjani na kulitangaza vyema taifa.

Aidha RC Makonda amewaomba Watanzania kuendelea kuipa sapoti Timu ya Taifa katika michuano mbalimbali kwakuwa Timu yetu imeonyesha uwezo mkubwa na anaamini inaweza kufika mbali.