Home Mchanganyiko KAMPUNI YA BAYER KUBORESHA KILIMO CHA MBOGA MBOGA

KAMPUNI YA BAYER KUBORESHA KILIMO CHA MBOGA MBOGA

0

 

Na.Vero Ignatus,Iringa.

Kampuni ya Bayer  Crop Science ambayo  zamani illiyokua ikijulikana kama Monsato  inayo jishughulisha na usambazaji na uzalishaji wa pembejeo za kilimo ikiwa ni pamoja na  viatilifu ,Mbegu za nafaka na  mboga mboga imedhamiria kuboresha kilimo  cha mboga mboga   Tanzania haswa kwa wateja wake wa nyanda za juu kusini.


 William Macha ni Mwakilishi wa kampuni ya Bayer Crop Science  akizungumza na wakulima katika Kijiji cha Ilula amesema   kuwa kwa sasa wana mbegu mpya za nyanya ambazo zinastahimili magonjwa na zimefanyiwa utafiti kwani kampuni hiyo   inaongoza duniani kwa kufanya na kuendeleza tafiti.

 Amesema kuwa Kitengo cha mboga mboga  SEMINIS ndio kinachozalisha na kujikita Zaidi katika kuzalisha mazao ya mboga mboga tofauti kama nyanya, vitunguu, hoho,kabichi, na kadhalika.


Kwa nyanda za juu kusini (Iringa na maeneo ya jirani) kampuni hii imefanya tafiti za kutosha  na hivyo kuwaletea wakulima wa Tanzania Mbegu bora ya nyanya iitwayo FIRENZE F1 inayotoa nyanya ijulikanayo kama “Nyanya DumDum” Alisema Macha

Mtokambali Mrisho ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakulima wa nyanya na mboga mboga  amesema kuwa kwa mara ya kwanza mbegu ya Firenze F1 kuingia, ilifanyiwa majaribio katika kijiji cha Tanangozi Iringa na kufanya vizuri sana baada ya hapo ilipendekezwa kuwa mbegu bora zaidi na wakulima walianza kuitumia na kupata matokea makubwa.


Mtokambali amesema kuwa kwa sasa wakulima kutoka mikoa ya Dodoma na Morogoro wanafika kujifunza kwenye shamba darasa la mbegu hizo ambazo  zimeleta mavuno pesa kwa wakulima wengi mko wa Iringa na viunga.

Muwakilishi wa kampuni akiwaeleza waandishi umuhimu wa mbegu ya Firenze F1 kwa kilimo cha nyanya na wakulima

 William Macha ambaye ni Muwakilishi wa kampuni ya  Bayer Crop Science Akiwa na Directors wa KeyMedia Ltd  Sarah &Hanna Keiya , kwa ajili ya kumpongeza mkulima mwenye bidii.

William Macha muwakilishi wa kampuni ya Bayer Crop Science Akiwa na Directors wa KeyMedia Ltd  Sarah &Hanna Keiya , kwa ajili ya kumpongeza mkulima mwenye bidii.

 Kampuni ya Bayer Crop science imeonyesha umuhimu wa michexo kwa wakulima kwa kuandaa tumu kutoka vijiji vya Iringa.