Home Mchanganyiko VIONGOZI WA SERIKALI NA WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA BRELA KATIKA MAONYESHO YA...

VIONGOZI WA SERIKALI NA WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA BRELA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM

0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akipata maelezo kwenye banda la Usajiri wa Leseni na Biashara (BRELA) alipolitembelea banda hilo na  kujionea huduma inayotolewa katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Buchweishaija  akimsikiliza Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu BRELA Bi.Loy Mhando wa kwanza upande wa kushoto na (katikati) ni Afisa habari na Mawasiliano Robertha Makinda alipotembelea banda la Usajiri wa Leseni na Biashara (BRELA) katika Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yanayofanyika  katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Afisa habari na Mawasiliano BRELA  Bi.Robertha Makinda,akiongea na wageni mbalimbali waliotembelea banda la Usajiri wa Leseni na Biashara (BRELA) katika Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yanayofanyika  katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Emmanuel Kakwezi akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la Usajiri wa Leseni na Biashara (BRELA) katika Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yanayofanyika  katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.