Home Mchanganyiko WAZIRI WA KILIMO MHE JAPHET HASUNGA AKUTANA NA MKURUGENZI MKAAZI WA USAID...

WAZIRI WA KILIMO MHE JAPHET HASUNGA AKUTANA NA MKURUGENZI MKAAZI WA USAID TANZANIA NDG ANDY KARAS, AMUELEZA MAMBO MAKUBWA MATANO

0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Tanzania Ndg Andy Karas katika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo Tarehe 1 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Cnal, Wizara ya Kilimo)

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na picha ya pamoja na mratibu wa mradi wa maboresho ya sera (ASPIRES) Prof David Nyange katika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo Tarehe 1 Julai 2019.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Tanzania Ndg Andy Karas katika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo Tarehe 1 Julai 2019. Wengine pichani ni Naibu Mkurugenzi wa ofisi ya ukuaji wa uchumi (USAID) Tanzania Bi Michelle Corzine, na Mtaalamu wa sera katika usimamizi wa miradi Ndg Semaly kisamo

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo – Dar es salaam

 

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo Tarehe 1
Julai 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la
 Marekani la
Maendeleo ya Kimataifa (
USAIDNdg Andy Karas katika Ofisi za Wizara ya Kilimo
Jijini Dar es salaam.

 

Katika
mazungumzo hayo Mhe Hasunga amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Wizara ya Kilimo
imejipanga kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ili kuondokana na
dhana ya kilimo cha kujikimu na kuhamia katika kilimo cha kibiashara. Waziri
Hasunga alisema kuwa ili kuongeza tija katika Kilimo, Wizara yake imejipanga
kuimarisha utafiti.

 

Alisema kuwa
maendeleo ya kilimo yanategemea zaidi utafiti hususani wa udongo vilevile
kubaini teknolojia bora itakayo pelekea kukisogeza kilimo katika hatua kubwa ya
mafanikio na kimageuzi.

 

Amesema kuwa
pamoja na mambo mengine wizara ya kilimo pia imejipanga katika kuongeza thamani
ya mazao ya kilimo kuliko kusafirisha pasina kuongeza thamani.

 

“Tukiongeza
thamani ni wazi kuwa uchumi utapanda, lakini zaidi ajira ziataongezeka kwa
wananchi, tutakuwa na Pato zuri la kigeni sambamba na utambulisho wa nchi” Alikaririwa
Mhe Hasunga

 

Kuhusu sekta
ya umwagiliaji Mhe Hasunga alisema kuwa Tanzania ina jumla ya Hekta zaidi ya
Milioni 29 zinazofaa katika umwagiliaji lakini ni hekta 475,000 ndizo ambazo
zimefanyiwa kazi.

 

“Kwa maana
hiyo kuna fursa kubwa katika umwagiliaji hivyo ninyi kama wadau kadhalika natoa
wito kwa wadau wengine kujitokeza kuwekeza katika umwagiliaji” Alisema

 

Kuhusu Lishe
Waziri Hasunga alisema kuwa wizara imeendelea kuweka hamasa kwa wakulima ili
kuwa na lishe bora. Aliongeza kuwa watanzania wanapaswa kuwa na utamaduni wa
kula vizuri ili kuondokana na magonjwa mbalimbali kama vile utapiamlo.

 

Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Marekani la
Maendeleo ya Kimataifa (
USAIDNdg Andy Karas ameipongeza serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
Magufuli kwa mikakati madhubuti ya kuimarisha sekta ya kilimo nchini.

 

Aidha, Karas
amemuomba Waziri wa Kilimo kuteua watu wawili kutoka wizarani watakaokuwa
kiungo muhimu baina ya serikali na miradi ya USAID sambamba na mtu
atakayeratibu mikutano ya wadau wa maendeleo.