Home Mchanganyiko TUME YA MADINI YANG’ARA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

TUME YA MADINI YANG’ARA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

0

*************

Leo tarehe 30 Juni, 2019 Tume ya Madini kwa kushirikiana na wadau wa madini imeendelea na utoaji wa elimu katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba kwa mwaka 2019 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Taasisi za Serikali zinazoshiriki katika banda la Tume ya Madini ni pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Masuala ya Madini na Gesi Asilia (TEITI)

Kampuni za madini zinazoshiriki katika Banda la Tume ya Madini ni pamoja na Williamson Diamonds Limited, Shanta Mining  Co. Limited, Geita Gold Mining Limited, TANSHEQ, Marmo & Granito Mines (T) Limited na Afro Gems Limited