Home Mchanganyiko UNILEVER WAKABIDHI VIFAA VYA KUHIFADHIA TAKA KWA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

UNILEVER WAKABIDHI VIFAA VYA KUHIFADHIA TAKA KWA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

0

Meneja wa Kiwanda cha Chai Kabambe Njombe -Unilever Alawi Sakay (Mwenye koti jeusi) akikabidhi vifaa vya kuhifadhia taka vyenye thamani ya Shilingi 1,500,000/= kwa umoja wa wafanyakazi wa Stendi Njombe ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuhakikisha kuwa mazingira ya Mji wa Njombe yapo katika hali ya usafi na kuepuka utupaji wa taka ovyo katika maeneo ya Mji.

Sehemu ya Wafanyakazi wanaofanya shughuli zao katika eneo la stendi kuu Njombe wakishuhudia tukio la kukabidhiwa kwa vifaa vya kuhifadhia taka kutoka Kiwanda cha Chai Kabambe -Unilever.

Katibu Tawala Wilaya Ndg. Emmanuel George akitoa shukrani zake kwa kiwanda cha Chai Kabambe na kuwaomba kuendelea kushirikiana katika kuweka Mji wa Njombe katika hali ya usafi.

Wafanyakazi stendi kuu Njombe mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya kuhifadhia taka kutoka katika Kiwanda cha Chai Kabambe-Unilever