Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja ABDALLAH BUSHIRI  @ SHIJA [42], mkazi wa Igodima Jijini Mbeya  kwa tuhuma za kufanya kazi za utabibu bila kuwa na taaluma ya utabibu hususani kwa magonjwa ya wanawake wenye matatizo ya uzazi.

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa hakuwa na kibali chochote cha kufanya shughuli hiyo wala cheti chenye taaluma hiyo na alikiri kuwatapeli wahanga hao pesa Tshs 2,472,000/= kwa madai kuwa atawasaidia. Hata hivyo alishindwa kutatua matatizo ya wahanga hao ikiwemo kupata ujauzito.

Katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa mtuhumiwa vilipatikana vifaa tiba na dawa za Hospitali za Serikali [MSD] kama ifuatavyo :-

 1. Fomu za Maabara / vipimo na kadi za Hospitali na Zahanati

 2. Urine Pregnant Test  [UPT] zipatazo 15.

 3. Dawa ya kusafisha vidonda aina ya EUSOL chupa 1

 4. Spirit chupa 1

 5. Iodine chupa 1

 6. Kipimo kimoja cha Maralia  “MRDT

 7. Glucose chupa moja iliyokwisha muda wake

 8. Dawa aina ya Metonidazole za MSD tano

 9. Dawa ya ganzi chupa 3

 10. Surgical blades 26

 11. BP Digital Machine 1

 12. Thermometer 1

 13. Canula 4

 14. Syringe 89

 15. Giving set 1

 16. Clinical Coat 1

 17. Gloves boksi 1

 18. Picha za X- Ray

 19. Madaftari ya kurekodi wagonjwa aliokuwa anawatibu.

MAFANIKIO:

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya katika kupambana na uhalifu na wahalifu kwa mujibu wa sheria za Nchi limeweza kupata mafanikio mbalimbali kama ifuatavyo;

Mnamo terehe 28/11/2018 majira ya saa 02:00 usiku huko eneo la lwambi Mjini Mbeya HABIB S/O MORIS  akiwa amelala nyumbani  kwake alivamiwa na vijana wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi ambao majina yao ni RICHARD S/O JACKSON ,Miaka 30, Mnyamwez, fundi ujenzi na mkazi wa DDC Mbalizi na DAVID S/O RABI MWASHINANI,miaka 32, Msafwa ,Mkulima  na Mkazi wa Mbalizi baada ya kuingia ndani walianza kumshambulia mhanga kisha kupora TV moja, Nguo mbalimbali  za kuvaa, Mabegi mawili na Viatu mbalimbali.

Msako uliendeshwa na tarehe 09/12/2018 watuhumiwa hao walikamatwa. Tarehe 06/01/2019 watuhumiwa walifikishwa Mahakamani ya Wilaya ya Mbeya CC No: 12/2019. Tarehe 26/06/2019 washitakiwa wote wawili wamepatikana  na hatia mbele ya Hakimu MTUMO  na kupewa adhabu kwenda jela miaka 30 kila mmoja na kuchapwa viboko sita wanapoingia gerezani.

[ULRICH O. MATEI  – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.