TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI Nchi za Kiafrika
zimeiomba China kuhakikisha kuwa ufadhili ama mikopo inayotoa kwa Nchi za
Kiafrika inalenga katika miradi ya kikanda itakayoziunganisha na kuzinufaisha
nchi hizo kiuchumi huku Tanzania ikiitaka China kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo
inayowekeza nchini iwe ya manufaa kwa pande zote mbili. Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb)
ameyasema hayo Beijing Nchini China katika mkutano wa waratibu wa jukwaa la
ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) alipopata fursa ya kuzungumza
katika mkutano huo na kuongeza kuwa endapo China itazisaidia kwa ufadhili ama
kwa mikopo nafuu kuwekeza katika miradi hasa ya miundombinu itakayoziunganisha
Nchi za kiafrika kwa kiasi kikubwa itazisaidia Nchi hizo kufanya biashara
zenyewe kwa zenyewe itaziwezesha kupiga
hatua za kimaendeleo na kiuchumi na hivyo kujitegemea. Ameongeza kuwa
Mkutano huo wa waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika
(FOCAC) umekuwa ni wa manufaa kwa kuwa Nchi zenyewe za kiafrika zimepata fursa
ya kutaja baadhi ya miradi ya kipaumbele kutokana na uitaji wa Nchi husika huku akiitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na
uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji kwa kuwa Nchi nyingi za Kiafrika bado zina
vyanzo vingi vya maji vinavyoweza kuzalisha umeme ambao utakuwa ni wa bei nafuu
na kusaidia katika ujenzi wa viwanda. Aidha katika
mkutano huo wa siku mbili uliozikutanisha Nchi zipatazo 53 za Kiafrika na China
zimeitaka China pia kuhakikisha inasaidia ama kufadhili katika kuinua uwezo wa
kitaaluma utakaowawezesha vijana kwa Kiafrika kujiajiri na kupata wataalam
wabobezi katika masuala mbalimbali kutokana na uwekezaji hasa wa viwanda na
miundombinu utakaofanywa kwa pamoja na China na Nchi za Kiafrika. Akizungumza mara
baada ya kumalizika kwa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amesema katika mkutano huo wa
waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) Tanzania
imesisitiza kuwa katika miradi ya uwekezaji,ya misaada ama ile ya mikopo nafuu
inayoelekezwa Tanzania iwe ni ile yenye manufaa kwa pande zote mbili yaani win
win situation kama anavyosisitiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli. Akisoma hotuba
kwa niaba ya Rais wa China Mhe. Xi Jimping, Waziri wa Mambo ya Nje wa China
Mhe. Wang Yi amesema kuwa China haitatoa misaada yenye masharti magumu kwa Nchi
za Afrika, badala yake itaendeleza ushirikiano wake na Afrika katika kutekeleza
miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa pande zote mbili. Katika hotuba
hiyo,serikali ya China imeahidi kuongeza umoja na ushirikiano kati yake na
Afrika katika masuala ya kikanda na kimataifa ikiwa ni pamoja na kudumisha
amani na usalama ili kuleta maendeleo
endelevu kwa watu na kuifanya dunia kuwa mahali salama pa kuishi. Mkutano huo wa
waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika limeazimia kwa pamoja
kutekeleza miradi ya kipaumbele kulingana na uhitaji wa kila nchi kwa kufuata
hatua nane zilizotangazwa katika mkutano wa wakuu wa nchi wa FOCAC uliofanyika
mwezi September 2018 jijini Beijing. Hatua hizo ni
pamoja na program ya kuendeleza viwanda kupitia ujenzi wa maeneo maalum ya
viwanda, ujenzi wa miundombinu ikiwemo nishati,reli,barabara na
bandari,sambamba na ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vitakavyosaidia kuzalisha
nguvu kazi ya viwandani. Imetolewa
na: Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, BEIJNG –
CHINA. Normal
0 false
false
false EN-US
JA
X-NONE
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0cm 5.4pt 0cm 5.4pt;
mso-para-margin:0cm;
mso-para-margin-bottom:.0001pt;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:12.0pt;
font-family:Calibri;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-ansi-language:EN-US;} 25 Juni 2019
|