Jaji Mkuu mstaafu Mh.Auguistine Ramadhan, akiongea na wanahabari pamoja na mawakili mbalimbali katika mafunzo kwa mawakili yalioandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania(THRDC) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam
Mratibu wa kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania(THRDC), Bw. Onesmo Olengurumwa akiongea na wanahabari pamoja na mawakili waliojitokeza katika mafunzo kwa mawakili hapa nchini.
Mawakili kutoka katika maeneo mbalimbali hapa nchini wakipata picha ya pamoja na Jaji mkuu Mstaafu Mh.Auguistine Ramadhani katika mafunzo kwa mawakili uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
****************
NA EMMANUEL MBATILO
Mawakili kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini wamekutana kwa pamoja kupeana mafunzo ya kuelimishana kwenye masuala ya haki za binadamu ambapo yamehudhuliwa na majaji mbalimbali ambayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam katika mafunzo hayo, Jaji Mkuu mstaafu Mh.Auguistine Ramadhani amesema kuwa mawakili ambao watapata mafunzo hayo wanatakiwa sio kila tatizo lazima ulipeleke mahakamani muhimu wazingatie haki za binadamu.
“Kuna kanuni nyingi sana za uchanguzi, uchaguzi unaendeshwa na binadamu hivyo kutakuwa na matatizo ya hapa na pale na si kila tatizo linaweza kufanya uchaguzi unaweza ukabatilishwa”. Amesema Mh. Ramadhani.
Kwa upande wake Mratibu wa kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania(THRDC), Bw. Onesmo Olengurumwa amesema kuwa kuwepo kwa mafunzo hayo kwa mawakili kutafanya uwepo wa jopo la mawakili ambalo litakuwa na faida kubwa kwa nchi yetu hasa kutetea haki za binadamu pale wanapoona haki hiyo haifuatwi.
Naye Bw.Pasience Mlowe kutoka chama cha wanasheria Tanzania societyamesema kuwa mara nyingi mawakili wamekuwa wakifanya kazi zao kwa masirahi binafsi bila kuangalia mahitaji ya jamii hivyo kwakuwa mawakili wapo kwaajili ya kutetea jamii ambao hawawezi kupaza sauti zao hivyo wao wanatakiwa kuwa msaada hasa kwa wale ambao hawajiwezi.