Home Mchanganyiko GAVANA SHILATU AWAPA ZAWADI BODABODA

GAVANA SHILATU AWAPA ZAWADI BODABODA

0

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Vijana wengi nchini wamejiajiri katika sekta isiyo rasmi ya uendeshaji wa Pikipiki almaarufu Bodaboda ili kuweza kuyaendesha maisha yao pamoja na wategemezi wao.

Katika hali ya kutambua mchango wao kwa jamii na kwa Taifa, Afisa Tarafa Mihambwe  Emmanuel Shilatu amewapa zawadi ya viakisi mwanga “Reflectors” bure kwa Bodaboda waliopo Tarafa ya Mihambwe ambao wana vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo  kwani wameonyesha utii na heshima kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuvinunua vitambulisho vilivyotolewa nae.

“Bodaboda inabidi muelewe Serikali ya Rais Magufuli inawapenda sana na ndio maana Leo hii tunawazawadia reflectors bure kabisa kwa wote mliomuunga mkono Rais Magufuli kwa kununua  vitambulisho vya Wajasiriamali vinavyouzwa kwa Tsh. Elfu ishirini tu. Serikali itahakikisha hamsumbuliwi wakati mnatimiza majukumu yenu, muhimu mzingatie sheria za usalama Barabarani.” Alisisitiza Gavana Shilatu huku akishangiliwa na Bodaboda.

Mpaka sasa kwenye Tarafa ya Mihambwe Bodaboda wa kata za Kitama, Miuta, Mihambwe na Mkoreha wameshapatiwa viakisi mwanga pamoja na kupewa Elimu ya usalama Barabarani toka kwa Askari wa usalama Barabarani (Trafiki) waliombatana nae kwenye ziara hiyo.