Home Mchanganyiko Matukio Katika Picha Ziara ya Viongozi wa TAGCO na Idara ya Habari...

Matukio Katika Picha Ziara ya Viongozi wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO Jijini Dodoma

0

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini  (TAGCO) Bi Sarah Kibonde akisisitiza umuhimu wa maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kutumia mbinu za kisasa katika kutangaza mafanikio ya Serikali , hayo yamejiri leo June 25, 2019 Jijini Dodoma wakati wa ziara ya ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO walipotembelea Tume  ya Maendeleo ya Ushirika kwa lengo la kujionea utendaji wa Kitengo Cha mawasiliano Serikalini cha Tume hiyo.

Naibu Msajili wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bw. Charles Malunde akisisitiza jambo kwa ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO walipotembelea  Tume hiyo wakati wa ziara ya kutembelea Taasisi na Mashirika ya Umma yaliyopo Dodoma ili kujionea utendaji kazi wa vitengo vya Mawasiliano Serikalini vya Taasisi hizo.

Ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO ukiwa kwenye picha ya pamoja na  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Mhandisi Dkt  Everest Makene (katikati).

Afisa Habari wa Jiji la Dodoma Bw. Denis   Gondwe akisisitiza jambo kwa ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO walipotembelea Jiji la Dodoma leo kwa lengo la kuona utendaji wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Jiji hilo.

Ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO ukiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Baltazar Ngowi leo Jijini Dodoma wakati wa ziara yakutembelea Kitengo cha mawasiliano Serikalini cha Jiji hilo ili kujionea utendaji wake.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini  (TAGCO) Bi Sarah Kibonde akifurahia jambo na Kaimu mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Baltazar Ngowi leo Jijini Dodoma wakati wa ziara ya  ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari- MAELEZO kutembelea Kitengo cha mawasiliano Serikalini cha Jiji hilo ili kujionea utendaji wake.

Muwakilishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza jambo kwa Naibu Msajili wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bw. Charles Malunde wakati wa ziara ya ujumbe wa Idara hiyo na Chama cha Maafisa  Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) leo Jijini Dodoma.

 Naibu Msajili wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bw. Charles Malunde akisisitiza jambo kwa  ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO walipotembelea Tume hiyo leo Jijini Dodoma.

(Picha zote  Frank Mvungi- MAELEZO)