Na.Alex Sonna,DodomaSERIKALI imesema ipo katika mchakato kufanya maboresho ya sekta ndogo ya haki jinai nchini ili kuendana na kasi kubwa ya mabadiliko duniani yanayotokea katika nyanja mbalimbali.Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Waziri wa katiba na sheria Balozi Augustine Mahiga, wakati alipokuwa akifungua mkutano wa maboresho ya sekta ndogo ya haki jinai uliowajumuisha wataalam kutoka wizara na taasisi mbalimbali nchini.Amesema kuwa wao kama serikali wanao wajibu wa kufanya maboresho mbalimbali ya sekta hiyo ya haki jinai ili kuendana na wakati ulipo sasa.“Ndugu washriki nchi yetu na dunia kwa ujumla zimeshudia kasi kubwa ya mabadiliko yatokanayo katika nyanja zote za maisha, kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kiteknolojia hali ambayo imesababisha kuwepo kwa mbinu mpya za uharifu ambazo ushughulikiaji wake unahitaji kuendana na mabadiloko hayo”amesema.Aidha amebainisha kuwa kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Wizara na wadau waliona umuhimu wa kufanya majadilinao ya pamoja kwa lengo la kuboresha sekta ndogo ya haki jinai.Amebainisha kuwa maboresho yanayotarajiwa yatajumuisha maeneo yote yenye changamoto yakiwemo ya kisera, kisheria na kiorganizesheni ili kuufanya mfumo huo kuweza kuakisi changamoto za maendeleo za kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.Pia amesema sekta hiyo ndogo ya haki jinai bado inakabiliwa na changamoto kama vile majengo ya mahakama ambayo yamejengwa toka wakati wa mkoloni.Ameongeza kuwa maboresho hayo yatasaidia katika kukidhi ongezeko la watu ambalo limekuwepo havi sasa nchini.Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju, amesema maboresho ya mfumo wa haki jinai yatasaidia kulifanya taifa kuwa na jamii ya watu waliostaarabika na kuheshimu utawala wa sheria pamoja na kutunza amani na utajiri wa rasilimali.“Marekebisho hayo yanasaidia katika kutengeneza taifa ambalo limestaarabika na kuwa na jamii ambayo inafuata na kuheshimu taratibu za nchi yao” amesema.Amebainisha mfumo wa haki jinai unafanya kazi kwa mfumo wa mnyororo wa taasisi katika kuhakikisha wananchi wanapata haki na kupambana na uharifu wa aina yeyote ukiwemo ule wa kimataifa.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga kufungua Kikao kazi Wakuu wa Taasisi za Haki Jinai kuhusu Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai kinachofanyika katika Hoteli ya St. Gasper jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kikao Kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga akisoma hotuba yake kabla ya kufungua kikao kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki jinai.
………………..