*****************
24,Juni
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
WATU wanne wamejeruhiwa baada ya kutokea ajali ya gari la abiria aina ya higer kampuni ya Hai express huko barabara kuu ya Dar es salaam -Morogoro,eneo la Kwamatias Kibaha .
Katika ajali hiyo dereva wa gari hiyo,Juma Abdallah alitoroka baada ya kusababisha ajali kizembe ,ambapo anatakiwa kujisalimisha katika jeshi la polisi mkoani humo ,kabla hajatafutwa.
Akielezea kuhusu ajali hiyo,kamanda wa polisi mkoani ,Wankyo Nyigesa alieleza imetokea majira ya saa 1:30 asubuhi Juni 24 mwaka huu.
Alisema, gari hilo la abiria lenye namba za usajili T.329 DGC ikiendeshwa na Juma alitoroka ikiwa na abiria 48 ikitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya,kupitia Kibaha Mji iliacha njia na kupinduka na kusababisha abiria wanne kupata majeraha.
Kati ya abiria hao watatu ni wanawake ambao wametibiwa na kuruhusiwa na mmoja mwanaume ambae anaendelea na matibabu katika hospital ya rufaa ya Tumbi .
“Chanzo cha ajali ni dereva wa gari hilo kujaribu kuyapita magari mengine barabarani katika eneo lililozuiliwa darajani hivyo kushindwa kulimudu na kuliangusha “alifafanua Wankyo.
Wankyo alibainisha ,alimtaka dereva huyo ajisalimishe mwenyewe ili achukuliwe hatua za kisheria.