Home Mchanganyiko KATIBU MKUU AALCO AITEMBELEA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA JIJINI DODOMA

KATIBU MKUU AALCO AITEMBELEA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA JIJINI DODOMA

0

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akiwa na Prof. Kennedy Gastorn (kushoto) na Prof. Sifuni Mchome (kulia) alipokutana na Prof. Gastorn ambaye ni Katibu Mkuu wa AALCO alipowatembelea Wizarani jijini DODOMA.

Prof Gastorn (kulia) akimkabidhi Prof.Mchome zawadi ya kitabu alichoandika kuhusu Afrika Mashariki.

Prof.Mchome akiagana na Prof.Gastorn aliyewatembelea katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma

……………………..

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (ASIA-AFRICAN LEGAL CONSULTATIVE ORGANISATION(AALCO) PROF. Kennedy Gastorn ameitembelea wizara ya Katiba na Sheria jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo Prof. Gastorn amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome  katika Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Prof. Gastorn na wenyeji wake wamezungumza masuala mbalimbali juu ya kuimarisha umoja huo na jinsi ya kunufaisha nchi wanachama.

AALCO ilianzishwa mwaka 1956 kwa lengo la kuwa chombo cha ushauri na ushirikiano katika masuala ya sheria za kimataifa kwa nchi za Asia na Afrika.

Toka kuanzishwa kwake AALCO imewezesha nchi wanachama kushirikiana na kubadilishana  uzoefu katika masuala mbalimbali ya sheria za kimataifa na kimechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sheria za kimataifa.

Tanzania ilijiungana umoja huo 1973 .

Prof. Gastorn ni Mtanzania  na alichaguliwa kushika nafasi hiyo Agosti 2016.