Home Michezo AMBOKILE ALAMBA DILI TP MAZEMBE

AMBOKILE ALAMBA DILI TP MAZEMBE

0

*******************

NA EMMANUEL MBATILO

Mshambuliaji wa kati ambaye alikuwa nakipiga katika klabu ya Mbeya City msimu uliopita Eliud Ambokile amekamilisha usajili wake kutoka Mbeya City kwenda TP Mazembe kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Mshambuliaji huyo amejiunga na klabu hiyo ambayo ililazimika kutokuingia mkataba na Ibrahim Ajibu kwa vigezo mbalimbali hivyo wakaamua kumchukua Ambokile

Ambokile anakuwa anaingia katika orodha ya wachezaji ambao wameichezea klabu hiyo ya TP Mazembe ambayo ilimuibua Mbwana Samata ambaye kwasasa hakamatiki barani Ulaya.