Home Michezo YANGA U20 YAICHAPA 2-0 SIMBA U20 NA KUMALIZA NAFASI YA TATU LIGI...

YANGA U20 YAICHAPA 2-0 SIMBA U20 NA KUMALIZA NAFASI YA TATU LIGI YA VIJANA U20

0

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Yanga SC imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Simba SC.
Ushindi huo wa Yanga SC umetokana na mabao ya wachezaji wake nyota, Kilaza Mazoea dakika ya 35 na Julius Wilson dakika ya 85 mchana wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
Wakati Yanga iliangukia kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu baada ya kufungwa na Azam kwa penalti 3-0 kufuatia sare ya 0-0, Simba SC ilichapwa 3-1 na Mtibwa Sugar katika mechi za Nusu Fainali hapo hapo Azam Complex.

Hicho kinakuwa kipigo pili Yanga U20 wanawapa watani wao wa jadi, Simba baada ya kipiga 2-1 kwenye mchezo wa Kundi A la michuano hii wiki iliyopita.