Home Michezo Waziri  Mwakyembe Amtambulisha kwa Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya...

Waziri  Mwakyembe Amtambulisha kwa Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo

0

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania Profesa Frowin Nyoni (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) kwenye Kikao cha kumtambulisha kwa Wajumbe wa Bodi hiyo Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo (kulia) katika Ukumbi wa mikutano wa Bodi hiyo iliyopo Mtaa wa Samora Posta jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimtambulisha kwa Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (hawapo pichani) Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo (kulia) kwenye Kikao cha kumtambulisha kwa Wajumbe wa Bodi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Filamu iliyopo Mtaa wa Samora Posta jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha kumtambulisha kwa Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo (kulia) katika Ukumbi wa mikutano wa Bodi hiyo iliyopo Mtaa wa Samora Posta jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Frowin Nyoni.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo (kulia) akimuelezea jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa kikao cha kumtambulisha kwa Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania Kaimu Katibu Mtendaji huyo katika Ukumbi wa mikutano wa Bodi hiyo iliyopo Mtaa wa Samora Posta jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania wakifurahia ujumbe wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) kwenye kikao cha kumtambulisha kwa Wajumbe wa Bodi hiyo Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo (hayupo pichani) katika Ukumbi wa mikutano wa Bodi hiyo iliyopo Mtaa wa Samora Posta jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wakwanza kushoto) akimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania (aliyenyoosha mkono) wakati akifafanua jambo kwenye kikao cha kumtambulisha kwa Wajumbe wa Bodi hiyo Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo katika Ukumbi wa mikutano wa Bodi hiyo iliyopo Mtaa wa Samora Posta jijini Dar es Salaam.

…………………………

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe mapema leo amekutana na Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania katika ofisi za Bodi ya Filamu na kumtambulisha kwa Wajumbe wa Bodi hiyo Kaimu Katibu Mtendaji mpya wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo.

Katika kikao hicho Mhe. Mwakyembe alipongeza jitihada chanya zilizoanza kufanywa na Naibu Katibu Mtendaji huyo katika kipindi kifupi cha kuteuliwa kwake na kumtaka kufanya kazi kwa bidii na weledi wa hali ya juu katika kuhakikisha Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza inasonga mbele na kuwa sehemu ya pato kwa Taifa na Wanatasnia wenyewe.

“Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ni moja ya Sekta kubwa na muhimu zinazoweza kukuza pato la nchi na kupunguza umaskini kwa raia wake, hivyo Bodi ya Filamu ni wajibu wenu kutengeneza mazingira rafiki yatakayo wezesha Sekta hii kukuwa hapa nchini na kupunguza umaskini kwa Watendaji wake” Dkt. Mwakyembe alisema.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji mpya wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo alimshukuru Waziri Mwakyembe kwa kushiriki katika kikao hicho cha kutambulishwa kwake kwa Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania na kumuahidi kuendelea kufanya kazi nzuri itakayoimarisha na kukuza Tasnia ya Filamu nchini kwa kushirikiana na Wajumbe hao wa Bodi ya Ushauri inayoongozwa na Mwenyekiti wake Profesa Frowin Nyoni, kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Filamu na kuimarisha umoja wa vyama vya Watendaji katika Filamu ili kuhakikisha Filamu inakuwa jukwaa rasmi la uchumi hapa nchini.

“kwa pamoja tutashirikiana katika kuifanya Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza inakuwa na mchango chanya kwa Taifa letu na sio sehemu au jukwaa la kuharibu maadili ya kitanzania, hivyo tunaahidi kuifanya Sekta hii kuzidi kuimarika ili iweze kuwa jukwaa la moja kwa moja la pato la mtu binafsi na Taifa kwa ujumla”. Dkt. Kilonzo alisema.

Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Filamu ina wajumbe 8 ikiongozwa na Mwenyekiti Profesa. Frowin Nyoni na Katibu Dkt. Kiagho Kilonzo ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini.