Home Mchanganyiko SERIKALI YAPIGA MARUFUKU VIFUNGASHIO VISIVYO NA UTAMBULISHO

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU VIFUNGASHIO VISIVYO NA UTAMBULISHO

0

Katibu Mtendaji wa NEMC Dkt Samweli Mwafyenga akitolea ufafanuzi jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari, walipokuwa wakitolea ufafanuzi mifuko laini iliyoibuka baada ya katazo la mifuko ya plastiki jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo, akionyesha vibebeo ambovyo vinatumika hivi sasa ambavyo haviruhusiwi Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Barozi Joseph Sokoine akitolea ufafanuzi jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari, walipokuwa wakitolea ufafanuzi mifuko laini iliyoibuka baada ya katazo la mifuko ya plastiki jijini Dodoma.

Baadhi ya vibebeo vinavyotumika sasa ambavyo vimepigwa marufuku kutumika kuanzia leo.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo, akionyesha kibebeo ambacho kimepigwa lakiri lakini hakina utambulisho wa mtengenezaji na ujazo wa bidhaa iliyomo ambavyo kwa sasa vimepigwa marufuku kutumika kuanzia leo.

………………………

Na.Alex Sonna, DODOMA.

SERIKALI imepiga marufuku matumizi ya mifuko laini yenye rangi nyeupe ambayo kwa sasa inatumika kama vifungashio na kubebea vya bidhaa, baada ya katazo la kutumia mifuko ya plastiki ambayo si salama kwa afya ya mlaji.

Huku ikiwataka wajasiliamali kuchangamkia fulsa hiyo kwa kutengeneza mifuko mbadala kwa mali ghafi za ndani kwani katazo la mifuko ya plastiki ni endelevu na serikali haita rudi nyuma.

Katazo hilo limetolewa leo jijini Dodoma, na katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhandisi Joseph Malongo, wakati akitoa tathmini ya katazo la mifuko ya plastiki na kutolea  ufafanuzi suala la kutumia mifuko mbadala.

Amesema ni marufuku  kutumia mifuko mweupe ya vifungashio ambayo haina rebo ya mtengenezaji na ukubwa na kiwango cha mfuko huo kwani  ni kinyume na sheria kutumia mifuko hiyo.

“Baada ya katazo la kutumia mifuko ya plastiki kuna mifuko imeibuka mweupe ukiangalia mifuko hii haina haina kiwango na si salama kwa mtumiaji kwa sababu ukiweka bidhaa humu na nafasi ya kutumbukiza kitu kingine ambacho kinaweza kumdhuru mlaji” amesema.

Amefafanua vifungashio vilivyoruhusiwa ni  vile ambavyo ambavyo vimefungwa kwa lakiri(vilivyo fungwa kwa siri) ambayo pia inajina la mtengenezaji mahali alipo, ukubwa wa kifungashio hicho na kutambulisha bidhaa iliyomo ndani.

Amesema tangu katazo la mifuko ya plastiki kuanza kutumika kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa mifuko mbadala lakini ofisi yake imekuwa ikifanya jitihada kubwa kukabiliana na tatizo  hilo.

Mpaka sasa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira imehamasisha wazalishaji wa mifuko mbadala kuunda chama chao ambacho kitasaidia katika kuhamasishana kuzalisha mifuko mbadala kukabiliana na changamoto ya uhaba wa mifuko mbadala.

Amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa wazalishaji  wa mifuko mbadala kuzalisha mifuko yenye viwango ambapo kwa kushirikiana na shirika la viwango Tanzania(TBS) na mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) wapo mbioni kukamilisha zoezi la kutoa viwango vya mifuko mbadala.

Amebainisha serikali itaendelea kutolea ufafanuzi wa matumizi sahihi ya mifuko mbadala, na alishauri wananchi kuweza kutumia mifuko ya karatasi ambayo haivujishi maji.

Amesema Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,  kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Dodoma na NEMC watafanya zoezi la kuondoa mifuko ya plastiki  iliyozagaa ovyo mitaani, na kusema kampeni hiyo itafanywa na ofisi  ya  NEMC kanda zote katika ngazi zote kutoka ngazi ya halmashauri hadi ngazi ya mitaa Tanzania nzima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Dkt Samweli Mwafyenga, amesema NEMC inaendelea na operation kabambe nchi nzima ya kusaka mifuko  ya plastiki ambayo imebadilishiwa matumizi yake na kukiuka sheria.

Amebainisha operation hiyo inahusisha vyombo vya ulinzi na usalama, kamati za ulinzi na usalama za Mikoa na Wilaya mamlaka za serikali za mitaa mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa Serikali, shirika la viwango Tanzania(TBS).

Mamlaka ya chakula na dawa(TFDA) Ofisi ya Taifa ya mashtaka pamoja na Mamlaka za viwanja vya ndage, Bandari, Forodha, uhamiaji na usafiri wan chi kavu kwa pamoja kuhakikisha kampeni hiyo ikafanikiwa na kuweka mazingira na afya za mlaji zinakuwa salama.

Amesema kwa kufanikisha hilo wamewakutanisha wenye viwanda vya kutengeneza mifuko mbadala wa ndani na wameunda kikundi cha wazalishaji wa ndani na tayari  kwa kushirikiana na SIDO wameagiza mashine.

“Katika kuimarisha viwanda vyetu vya ndani nimeamua kuwakutanisha wenye viwanda vya kutengeneza mifuko hii, na tumeunda vikundi ili na kwa kushirikiana na SIDO tumeagiza mashine za kutengeneza mifuko mbada toka India na vinawasili hivi karibuni” amesema.

Serikali ilitangaza April mosi, 2019, juu y katazo la  matumizi ya mifuko ya plastiki na kuanza kutumika rasmi Juni mosi mwaka  huu.