Home Mchanganyiko HASSAN KESSY ARUHUSIWA KUICHEZEA TAIFA STARS DHIDI YA SIMBA WA TERENGA JUMAPILI

HASSAN KESSY ARUHUSIWA KUICHEZEA TAIFA STARS DHIDI YA SIMBA WA TERENGA JUMAPILI

0

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemruhusu beki wa timu ya soka ya taifa Taifa Stars,Hassan Kessy,kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Senegal,utakaofanyika Juni 23,katika  Uwanja wa 30 June Cairo,nchini Misri.

Maamuzi hayo ya CAF ya kumruhusu Kessy kucheza mchezo dhidi ya Senegal ni baada ya kujiridhisha,kuwa kadi mbili za njano, ambazo zilikuwa awali zinasemekana zingemfanya asicheze mchezo huo zilishaisha katika mchezo namba 101 ambao ulikuwa ni dhidi Cape Verde nyumbani.

Kutokana na taarifa hiyo ,Kocha Emmanuel Amuneke,anaweza kumtumia Kessy katika mchezo huo wa kwanza wa kombe la  Mataifa Afrika (AFCON) bila tatizo lolote kama atakuwa yupo kwenye progarmu yake.

Ikumbukwe kuwa.kesi alipata kadi mbili za njano katika michezo  miwili ya ugenini dhidi ya Uganda Cranes na Cape Verde,ambazo zilimalizika na kumfanya adhabu yake ya kutocheza iweze kuisha baada ya kusimama namba 101.