Home Michezo ALLY ALLY ASAINI YANGA MKATABA WA MIAKA MIWILI

ALLY ALLY ASAINI YANGA MKATABA WA MIAKA MIWILI

0

Beki kiraka wa timu ya KMC, Ally Ally ‘Mwarabu’  amejiunga na mabingwa wa kihistori Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya KMC

Ally amekuwa bora ndani ya KMC hali iliyomvutia Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera na kuacha maagizo kwamba naye aongezwe kwa wachezaji wa ndani.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa mipango ya usajili inaendelea kwa sasa kwa wachezaji wa ndani kwani wale wa kigeni wamekamilisha maagizo ya mwalimu kwa asilimia 90.