Home Mchanganyiko NAIBU KATIBU MKUU,WIZARA YA MAJI AONGOZA TIMU YA WATAALAM KUKAGUA ENEO LA...

NAIBU KATIBU MKUU,WIZARA YA MAJI AONGOZA TIMU YA WATAALAM KUKAGUA ENEO LA KAZI LA WABUNIFU MKOANI NJOMBE

0

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Emmanuel N.M Kalobelo (kati kati) akiongoza timu ya wataalam wakiwa katika eneo la kazi la wabunifu mkoani Njombe Bw. John Akani Fute na Bw. Jairo Ngairo.
Tukio hilo ni ufuatiliaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa tarehe 13 Juni, 2019 baada ya kukutana na wabunifu hao Ikulu jijini Dar es Salaam. Maelekezo kuhusu wabunifu hao yalielekezwa kwa Wizara na Taasisi zinazohusika kufuatilia na kutoa ushauri na kuona namna bora ya kuongeza tija.
Timu iliyotembelea wabunifu iliundwa na wataalam wa sekta za maji, nishati na elimu.

Wabunifu hao kutoka mkoani Njombe kazi zao zimejikita katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia nguvu ya maji na uundaji wa pampu za kusukuma maji.