Home Mchanganyiko ULEGA KUFUNGA MAONESHO YA GWARIDE LA MIFUGO DODOMA

ULEGA KUFUNGA MAONESHO YA GWARIDE LA MIFUGO DODOMA

0

Katibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Prof.Elisante Ole Gabriel,akiwasili katika kukagua maandalizi ya kesho kufunga maonesho ya gwaride la ng’ombe bora nchini ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mhe.Abdalah Ulega

Katibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Prof.Elisante Ole Gabriel,akimsikiliza Meneja wa Tawi la Dodoma Bw.Dickson Raymond  toka Kampuni ya Poly Machinery Co.Ltd akiwa anakagua maandalizi ya kesho kufunga maonesho ya gwaride la ng’ombe bora nchini ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mhe.Abdalah Ulega

Katibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Prof.Elisante Ole Gabriel,akicheza na vijana ambao walikuwa wakitoa burudani alipokuwa ameenda   kukagua maandalizi ya kesho kufunga maonesho ya gwaride la ng’ombe bora nchini ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mhe.Abdalah Ulega

Katibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Prof.Elisante Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kukagua maandalizi ya kesho ya ufugaji maonesho ya gwaride la ng’ombe bora nchini ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mhe.Abdalah Ulega.

Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdalah Ulega anatarajiwa kufunga maonesho ya gwaride la ng’ombe bora nchini kesho saa mbili na nusu.

Maonesho hayo ambayo yanayoendelea  jijini Dodoma katika viwanja vya maonesho ya nane nane yakiwa na lengo la kuongeza hamasa katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa Maziwa.

Akizungumzia maonesho hayo Katibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Prof.Elisante Ole Gabriel amesema kuwa Tanzania ni kati ya nchi zenye Ng’ombe wengi hivyo kuna haja ya kuboresha mifugo hiyo.

Katibu huyo amesema kuwa maandalizi ya maonesho hayo yanayofanyika kitaifa na kwa mara ya kwanza ni kutia hamasa ya kuwafanya watanzania kuacha kujivuna kuwa na wingi wa mifugo bali wawe na mifugo ambayo ina uzito mkubwa.

Aidha amesema kuwa  lengo la maonesho hayo ni kuwaonesha wananchi jinsi sayansi inavyofanywa kuhusu wanyama ili waweze kufahamu kuwa afya ya wanyama ni jambo kubwa na la muhimu.