Home Michezo TAIFA STARS YATOA SARE 1-1 NA ZIMBABWE MECHI YA KIRAFIKI MISRI

TAIFA STARS YATOA SARE 1-1 NA ZIMBABWE MECHI YA KIRAFIKI MISRI

0

Mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu akitafuta maarifa ya kumpita mchezaji wa Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki Jumapili Uwanja wa El Sekka El Hadid mjini Cairo. Timu hizo zilitoka 1-1, huo ukiwa mchezo wa pili kwa Taifa Stars wa kujipima nguvu katika kambi yake nchini Misri kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baadaye mwezi nchini humo, kufuatia kufungwa 1-0 na wenyeji wa michuano hyo, Mafarao Alhamisi.