Home Michezo RC MAKONDA AANZA SAFARI YA KUTIMIZA AHADI YA KUWAKABIDHI ENEO TIMU YA...

RC MAKONDA AANZA SAFARI YA KUTIMIZA AHADI YA KUWAKABIDHI ENEO TIMU YA YANGA.

0

*********************************

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameanza safari ya kutimiza ahadi yake kwa Wanayanga ambapo mapema leo amekutana na uongozi wa Timu ya soka ya Yanga chini ya Mwenyekiti wa Timu hiyo Dr. Mbette Msolla kwaajili ya kupokea nyaraka (document) mbalimbali za timu zitakazotumika kutengeneza hati ya Eneo aliloahidi kuwakabidhi.

RC Makonda amesema kuwa tayari eneo limepatikana Wilaya ya Kigamboni kama alivyoahidi na kinachofuata ni hatua za kuandaa hati ili aweze kuwakabidhi siku yoyote kuanzia sasa.

Itakumbukwa Jumamosi ya Juni 15 kwenye zoezi la kuchangia timu ya Yanga RC Makonda alitoa ahadi ya kutoa Eneo kwa timu hiyo.