*********************
Mfanyabiashara maarufu hapa nchini ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Igunga mkuani Tabora, Mh.Rostam Azizi ameweza kutoa kiasi cha shiringi Milioni 200 za kitanzania katika Tamasha la Kubwa Kuliko lililokuwa likifanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Hata hivyo katika tamasha hilo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa kiasi cha shilingi Milioni 10 ili kuweza kuichangia klabu hiyo kufikisha malengo ambayo wamejiwekea.
Katika Tamasha hilo Klabu ya Yanga ilitumia fursa hiyo kuwatangaza wachezaji wao wapya ambao waliwasajili siku chache zilizopita ambao ni Abdulaziz Makame pamoja na Balinga Juma ambaye msimu uliopita katika ligi ya nchini Uganda alikuwa mfungaji bora wa ligi Kuu.